• HABARI MPYA

    Thursday, October 08, 2015

    STAR TV WAONGEZA NEEMA LIGI DARAJA LA KWANZA TZ BARA

    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo limeingia mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya shilingi milioni mia nne hamsini (450,000,000), na kituo cha luninga cha Star Tv kurusha matangazo ya Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL)
    Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliishukuru kampuni ya Sahara Media Group kwa kuamua kuwekeza katika mpira wa miguu nchini kwa kuamua kuonyesha ligi daraja la kwanza.
    Malinzi ameviomba vilabu vya FDL kutumia udhamini huo kama chachu ya mafanikio na kufanya vizuri katika ligi hiyo itakayotoa timu tatu za kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (FDL) msimu ujao.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Star TV, Samuel Nyalla

    Aidha Malinzi amewaomba wamiliki wa viwanja vinavyotumika kwa michezo ya FDL kuviweka katika hali nzuri ya matunzo ili mechi zinazochezwa katika viwanja hivyo ziweze kuwa nzuri kiufundi na muonekano wa kwenye Luninga.
    Jumla ya udhamini wa Ligi Daraja la Kwanza kwa sasa ni shilingi bilioni moja na milioni mia tatu hamsini (1,350,000,000) ikiwa ni udhamini wa milioni mia tisa (900,000,000) kutoka StarTimes  mdhamini mkuu wa FDL na milioni mia nne hamsini (450,000,000) kutoka StarTv.
    Naye Makamu Mwenyekiti wa Sahara Media Group, Samwel Nyala ameishukuru TFF kwa kuwapa nafasi hiyo ya haki za matangazo kampuni yake kwa michezo ya Ligi Daraja la kwanza nchini (FDL).
    Katika kuhakikisha michezo hiyo inaonekana kwa wingi zaidi, Nyala alisema watafungua mkondo (Channel) ya Star Sports Plus itakayokua itakayokuwa inaonyesha michezo tu ikiwemo ligi daraja la kwanza (FDL).
    Akiongea kwa niaba ya vilabu ya ligi daraja la kwnza nchini (FDL), Asha Kigundula - Afisa habari wa klabu ya Friends Rangers ya jijini Dar es salaam, ameishukuru TFF kwa kuweza kuwapatia udhamini kwenye ligi, jambo ambalo litawapelekea kujiandaa na kufanya vizuri katika ligi msimu huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAR TV WAONGEZA NEEMA LIGI DARAJA LA KWANZA TZ BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top