• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 17, 2015

  ARSENAL YAITANDIKA WATFORD 3-0, SANCHEZ ‘KAMA KAWA’

  MATOKEO LIGI KUU ENGLAND LEO
  Oktoba 17, 2015  
  Watford 0-3 Arsenal
  West Bromwich Albion 1-0 Sunderland
  Manchester City 5-1 Bournemouth
  Everton 0-3 Manchester United
  Southampton 2-2 Leicester City
  Chelsea 2-0 Aston Villa
  Crystal Palace 1-3 West Ham United
  Tottenham Hotspur 0-0 Liverpool
  Kesho; Oktoba 18, 2015
  Newcastle United v Norwich City
  J’tatu Oktoba 19, 2015
  Swansea City v Stoke City 
  Alexis Sanchez wa Arsenal akishangilia baada ya timu yake bao dhidi ya Watford PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  ARSENAL imeng’ara katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga mabao 3-0 Watford Uwanja wa Vicarage Road usiku huu.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Alexis Sanchez dakika ya 62, Olivier Giroud dakika ya 68 na Aaron Ramsey dakika ya 74.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya England uliomalizika hivi karibuni, West Bromwich Albion wameshinda 1-0 dhidi ya Sunderland, bao pekee la Saido Berahino dakika ya 54 Uwanja wa The Hawthorns.
  Mechi zilizotangulia leo, Manchester City imeichapa mabao 5-1 Bournemouth Uwanja wa Etihad, Raheem Sterling akifunga matatu peke yake.
  Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Sterling alifunga mabao yake dakika saba 29 na 48, wakati mabao mengine ya City yamefungwa na Wilfried Bony dakika ya 11 na 89, wakati la Bournemouth la kufutia machozi limefungwa na Glenn Murray dakika ya 22.
  Mashetani Wekundu, Manchester United wameng’ara ugenini baada ya kuitandika Everton mabao 3-0 Uwanja wa Goodison Park, wafungaji  Morgan Schneiderlin dakika ya 18, Ander Herrera dakika ya 22 na Nahodha Wayne Rooney aliyeiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 62.

  Saido Berahino akipambana leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Southampton imelazimishwa sare ya 2-2 Leicester City, mabao yake yakifungwa na Jose Fonte dakika ya 21 na Virgil van Dijk dakika ya 37, wakati ya wapinzani wao yamefungwa na Jamie Vardy dakika ya 66 na Jamie Vardy dakika ya 91 Uwanja wa St. Mary's.
  Mabingwa watetezi, Chelsea wameshinda 2-0 dhidi dhidi ya Aston Villa mabao ya Diego Da Silva Costa dakika ya 34 na Alan Hutton aliyejifunga dakika ya 54 Uwanja wa Stamford Bridge.
  West Ham United imeshinda ugenini 3-1 dhidi ya Crystal Palace, mabao yake yakifungwa na Carl Jenkinson dakika ya 22, Manuel Lanzini dakika ya 88 na Dimitri Payet dakika ya 94, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji limefungwa na Yohan Cabaye kwa penalti dakika ya 25 Uwanja wa Selhurst Park.
  Kocha mpya wa Liverpool, Mjerumani Jurgen Klopp ameanza na sare tasa ugenini, baada ya kutoka 0-0 na Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane.
  Ligi Kuu ya England itaendelea kesho Newcastle United wakiikaribisha Norwich City Uwanja wa St. James' Park, wakati keshokutwa Swansea City watakuwa wenyeji wa Stoke City Uwanja wa  Liberty.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAITANDIKA WATFORD 3-0, SANCHEZ ‘KAMA KAWA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top