• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 31, 2015

  DROGBA KUREJEA ULAYA BAADA YA KUNG'ARA LIGI YA MAREKANI

  MWANASOKA bora wa zamani Afrika na gwiji wa klabu ya Chelsea ya England, Didier Drogba anaweza kurejea Ulaya ifikapo Januari mwakani, kutokana na kutakiwa na klabu ya Serie A, Bologna kwa mkopo kutoka Montreal Impact.
  Taarifa nchini Italia zinasema mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 ameivutia Bologna baada ya kufunga mabao 12 tangu amejiunga na klabu ya Canada Julai mwaka huu, ilikiwemo moja katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Toronto usiku wa Alhamisi.
  Montreal Impact inamilikiwa na Joey Saputo ambaye pia ana hisa nyingi na ni Mwenyekiti wa Bologna na gazeti la Corriere dello Sport limeripoti leo kwamba, mfanyabiashara huyo Canada anatumai Drogba atakubali kuhamia Italia.
  Drogba amefunga mabao 12 katika mechi kadhaa alizoichezea Montreal Impact tangu ajiunge nayo Julai

  Imekuwa kawaida kwa nyota wa Ligi Kuu ya Marekani, maarufu kama Major League Soccer kuhamia Ulaya kwa mkopo wakati wa mapumziko ya MLS na Saputo ameripotiwa kutaka mchezaji huyo wa Ivory Coast akaisaidie Bologna katika vita ya kukataa kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DROGBA KUREJEA ULAYA BAADA YA KUNG'ARA LIGI YA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top