• HABARI MPYA

  Saturday, October 24, 2015

  TAIFA STARS KUWEKA KAMBI OMAN KUJIANDAA NA ALGERIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaweka kambi Oman kwa maandalizi ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria mwezi ujao.
  Hayo yamefikiwa jana katika cha Kamati ya Taifa Stars hoteli ya Serena, Dar es Salaam, ingawa pendekezo hilo itabidi likubaliwe na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na kocha Charles Boniface Mkwasa.
  Habari ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imezipata, zimesema kwamba Kamafi imefanikiwa kupata kambi Oman na wazo litawasilishwa TFF kwa maamuzi ya mwisho.
  Wakati huo huo, Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda ameendelea kuwahamasisha Watanzania kuendelea kuichangia timu hiyo.
  Kikosi cha Taifa Stars

  "Mtanzania yeyote anaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (Sh100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi," amesema.
  Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Algeria Novemba 14, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana Novemba 17 mjini Algiers katika hatua ya mwisho ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi. 
  Tanzania ilipata nafasi hiyo baada ya kuitoa Malawi katika hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 Dar es Salaam na kufungwa 1-0 Blantyre.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUWEKA KAMBI OMAN KUJIANDAA NA ALGERIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top