• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 20, 2015

  ARSENAL NA BAYERN HAPATOSHI EMIRATES LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA , MOURINHO...

  RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA WIKI HII
  Leo Oktoba 20, 2015
  Bayer 04 Leverkusen v Roma Bay
  Arsenal v  Bayern Munich
  Zenit St Petersburg v Lyon
  Valencia v KAA Gent
  FC Porto v Maccabi Tel Aviv
  Dynamo Kyiv v Chelsea
  Dinamo Zagreb v Olympiakos
  BATE Borisov v Barcelona
  Kesho, Oktoba 21, 2015
  Juventus v Borussia Monchengladbach
  CSKA Moscow v Manchester United
  VfL Wolfsburg v PSV 
  Paris Saint-Germain v Real Madrid
  Manchester City v Sevilla
  Malmo FF v Shakhtar Donetsk
  Galatasaray v Benfica
  Atletico de Madrid v  FC Astana

  Kipa wa Arsenal, Petr Cech anatarajiwa kuanza leo dhidi ya Bayern Munich PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  KLABU ya Chelsea itawakosa washambuliaji wake Pedro na Loic Remy katika mchezo wa leo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev nchini Ukraine.
  Kocha Jose Mourinho amewaambia Waandishi wa Habari jana kwamba wachezaji wote hao wawili wana jajeruhi madogomadogo na itakuwa hatari kuwatumia dhidi ya vinara hao wenza wa Kundi G.
  "Wao (Pedro na Remy) wana majeruhi madogo madogo, wote na si maumivu makubwa, lakini hiwezekanikwa wao kucheza, wanacheza katika nafasi ambazo tuna wachezaji mbadala, hivyo hatuwezi kuwatoa mhanga,"amesema Mourinho.

  Kocha Jose Mourinho amesafiri hadi Ukraine kuwafuata Dynamo Kiev katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Kwa ujumla michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaendelea inaendelea leo, Bayer 04 Leverkusen ikiikaribisha Roma Uwanja wa BayArena mchezo wa Kundi E, Arsenal ikiwa mwenyeji wa Bayern Munich Uwanja wa Emirates mchezo wa Kundi F na Zenit St Petersburg wakiikaribisha Lyon Uwanja wa Petrovski mchezo wa Kundi H.
  Mechi nyingine za leo, Valencia CF watakuwa wenyeji wa KAA Gent Uwanja wa Mestalla mchezo wa Kundi H pia, FC Porto watakuwa wenyeji wa Maccabi Tel Aviv Uwanja wa Estadio do Dragao mchezo wa Kundi G, Dinamo Zagreb na Olympiakos Uwanja wa Maksimir mchezo wa Kundi F na BATE Borisov na Barcelona Uwanja wa Borisov Arena mchezo wa Kundi E.
  Mechi nyingine zitachewa kesho Juventus wakiikaribisha Borussia Monchengladbach Uwanja wa Juventus mchezo wa Kundi D, CSKA Moscow wakiwa wenyeji wa Manchester United Uwanja wa Arena Khimki mchezo wa Kundi B, VfL Wolfsburg wakiikaribisha PSV Uwanja wa Volkswagen Arena mchezo wa Kundi B pia na Paris Saint-Germain wakiwa wenyeji wa Real Madrid Uwanja wa Parc des Princes mchezo wa Kundi A.
  Uwanja wa Etihad, Manchester City wataikaribisha Sevilla mchezo wa Kundi D, Malmo FF wataikaribisha Shakhtar Donetsk Uwanja wa Swedbank mchezo wa Kundi A pia, Galatasaray watakuwa wenyeji wa Benfica Uwanja wa  Turk Telekom Arena mchezo wa Kundi C na Atletico Madrid wataikaribisha FC Astana Uwanja wa Vicente Calderon.

  Gwiji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry akikimbia kushangilia baada ya kufunga dhidi ya Bayern Munich mwaka 2005 

  REKODI YA ARSENAL NA BAYERN MUNICH
  2000/2001 Ligi ya Mabingwa
  Arsenal 2-2 Bayern Munich
  Bayern Munich 1-0 Arsenal
  2004/2005 Ligi ya Mabingwa
  Bayern Munich 3-1 Arsenal
  Arsenal 1-0 Bayern Munich
  2012/2013 Ligi ya Mabingwa
  Arsenal 1-3 Bayern Munich
  Bayern Munich 0-2 Arsenal 
  2013/2014 Ligi ya Mabingwa
  Arsenal 0-2 Bayern Munich
  Bayern Munich 1-1 Arsenal
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL NA BAYERN HAPATOSHI EMIRATES LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA , MOURINHO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top