• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 20, 2015

  BALE MUINGEREZA PEKEE TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA, MOURINHO NA WENGER WAINGIA 10 BORA KOCHA BORA WA DUNIA

  WINGA wa Wales, Gareth Bale ni Muingereza pekee aliyepenya katika orodha ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or kwa mwaka wa tatu mfululizo.
  Bale ni miongoni mwa wachezaji 11 wanaocheza Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga walioingia katika orodha hiyo ambayo ina wengine watano wa Ligi Kuu ya England na watano wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga.
  Wachezaji watatu wa Manchester City, Sergio Aguero, Kevin De Bruyne na Yaya Toure wameingia kwenye orodha hiyo sambamba na winga wa Chelsea, Eden Hazard na Alexis Sanchez, ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika klabu yake, Arsenal na kuipa mafanikio timu yake ya taifa, Chile katika Copa America mwaka 2015.

  Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale ni Muingereza pekee aliyeingia katika orodha ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mfaransa Arsene Wenger na Mreno Jose Mourinho wote wameingia kwenye 10 bora ya tuzo za kocha bora wa dunia, sambamba na kocha wa mabingwa wa Ulaya, Barcelona Luis Enrique na wa Bayern Munich, Pep Guardiola.
  Kocha wa Chile, Jorge Sampaoli ni kocha pekee wa timu ya taifa kwenye orodha hiyo, ambayo pia inahusisha makocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, Unai Emery wa Sevilla, Laurent Blanc wa PSG, Diego Simeone wa Atletico Madrid na Carlo Ancelotti, aliyeondoka Real Madrid baada ya msimu uliopita.
  Chelsea boss Jose Mourinho is on the shortlist for coach of the year 
  Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameingia kwenye orodha ya kuwania tuzo ya kocha bora wa mwaka 

  WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA

  WANAOWANIA BALLON D'OR: Sergio Aguero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale (Wales/Real Madrid), Karim Benzema (Ufaransa/Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid), Kevin De Bruyne (Ubelgiji/Manchester City), Eden Hazard (Ubelgiji/Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris St Germain), Andres Iniesta (Hispania/Barcelona), Toni Kroos (Ujerumani/Real Madrid), Robert Lewandowski (Poland/Bayern Munich), Javier Mascherano (Argentina/Barcelona), Lionel Messi (Argentina/Barcelona), Thomas Muller (Ujerumani/Bayern Munich), Manuel Neuer (Ujerumani/Bayern Munich), Neymar (Brazil/Barcelona), Paul Pogba (Ufaransa/Juventus), Ivan Rakitic (Croatia/Barcelona), Arjen Robben (Uholanzi/Bayern Munich), James Rodriguez (Colombia/Real Madrid), Alexis Sanchez (Chile/Arsenal), Luis Suarez (Uruguay/Barcelona), Yaya Toure (Ivory Coast/Manchester City), Arturo Vidal (Chile/Bayern Munich).
  WANAOWANI KOCHA BORA WA MWAKA: Massimiliano Allegri (Juventus), Carlo Ancelotti (Alikuwa Real Madrid), Laurent Blanc (Paris St Germain), Unai Emery (Sevilla), Pep Guardiola (Bayern Munich), Luis Enrique (Barcelona), Jose Mourinho (Chelsea), Jorge Sampaoli (Chile), Diego Simeone (Atletico Madrid) na Arsene Wenger (Arsenal).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALE MUINGEREZA PEKEE TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA, MOURINHO NA WENGER WAINGIA 10 BORA KOCHA BORA WA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top