• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 30, 2015

  CHEKA KUZIPIGA NA HILI JAMAA LA UINGEREZA DESEMBA MJINI MANCHESTER

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BONDIA wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo.
  Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.

  Mpinzani wa Cheka; Murray akishangilia na kocha wake, Oliver Harrison (kushoto) baada ya kumshinda Jorge Navarro

  Kwa mujibu wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.
   “Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano hilo, kuna vitu fulani fulani vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7 na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa sasa yupo Kenya kikazi.
  Alisema kuwa Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
  Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa
   “Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.
  Francis Cheka atakwenda kupigana Uingereza Desemba mwaka huu

  Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.
  Wakati huo huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku, hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuhairishwa dakika za mwisho.
  Ndambile alisema kuwa Mwakalebela alitakiwa kupambana na bondia Craig Kennedy na pambano hilo limefutwa kutokana na sababu za kiufundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHEKA KUZIPIGA NA HILI JAMAA LA UINGEREZA DESEMBA MJINI MANCHESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top