• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 17, 2015

  SIMBA SC KUFUTA UTEJA KWA MBEYA CITY YA BOBAN LEO?

  MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA WIKIENDI HII
  Okotba 17, 2015
  Yanga SC Vs Azam FC
  Majimaji FC Vs African Sports
  Mbeya City Vs Simba SC
  Ndanda FC Vs Toto Africans
  Stand United Vs Prisons
  Coastal Union Vs Mtibwa Sugar
  Oktoba 18, 2015
  Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar
  Mwadui FC Vs JKT Ruvu
  Winga wa Mbeya City, Idrisa Rashid (kushoto) akipambana na beki wa Simba SC, Abdi Banda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  REKODI YA SIMBA SC NA MBEYA CITY LIGI KUU

  April 18, 2015
  Mbeya City 2-0 Simba   
  Januari 28, 2015
  Simba 1-2 Mbeya City     
  Februari 15, 2014
  Mbeya City 1-1 Simba      
  Septemba 21, 2013
  Simba 2-2 Mbeya City 
  Na Princess Asia, MBEYA
  MBEYA City FC leo wanaanza rasmi maisha bila kocha wao, Juma Mwambusi aliyehamia Yanga SC- watakapomenyana na wakongwe, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
  Mbeya City inakutana na Simba SC ikiwa na maumivu mara mbili, kwanza kumpoteza kocha wake, Mwambusi aliyekwenda kuwa Msaidizi wa Mholanzi, Hans van der Pluijm Yanga SC na pia, Nahodha wake Juma Nyosso aliyefungiwa miaka miwili.
  Lakini habari njema tu ni kwamba, leo inaweza kumtumia kwa mara ya kwanza mchezaji wake mpya, Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ aliyewahi kuchezea Simba SC.
  Boban amesajiliwa na Mbeya City msimu huu, lakini akachelewa kujiunga na kikosi kwa sababu ambazo hazijulikani kabla ya wiki hii kutambulishwa amejiunga na timu.
  Kocha Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr leo akakosa huduma ya kinara wake wa mabao, Mganda Hamsi Kizza ‘Diego’ ambaye ni majeruhi, lakini Nahodha Mussa Hassan Mgosi yuko tayari kwa mchezo huo.
  Msimu huu, Simba SC inaonekana kuwa vizuri kuliko Mbeya City, kwani imepoteza mechi moja tu dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC wakati timu ya Mbeya imeshinda mechi moja tu, ikitoa sare moja na kufungwa mara nne.
  Kati ya mechi hizo, moja imefungwa nyumbani na Kagera Sugar 1-0 maana yake, si ajabau hata leo wakifungwa na Simba SC nyumbani.   
  Lakini ikumbukwe, Simba SC hawajawahi kuifunga Mbeya City tangu ipande Ligi Kuu, msimu wa kwanza wakitoa sare mechi zote na msimu uliopita Wekundu wa Msimbazi wakifungwa mechi zote. 
  Je, leo Simba SC iko tayari kufuta uteja kwa Mbeya City? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUFUTA UTEJA KWA MBEYA CITY YA BOBAN LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top