• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 26, 2015

  RIGOBERT SONG KOCHA MPYA WA CHAD ITAKAYOMENYANA NA STARS MACHI

  Song kushoto akizungumza na Mmoja wa Wakurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa Februari mwaka 2013 mjini Dar es Salaam 
  SHIRIKISHO la Soka Chad (CFF) limemteua gwiji wa Cameroon, Rigobert Song kuwa kocha wao mpya, akichukua nafasi ya Emmanuel Tregoat aliyefukuzwa.
  Song mwenye umri wa miaka 39 sasa, alistaafu soka ya ushindani mwaka 2011 na tangu hapo amekuwa akifanya kazi za uchambuzi kwenye TV. 
  Amethibitishwa leo kuwa kocha mpya wa Chad, ambayo ipo kundi moja G na Tanzania, Misri na Nigeria katika kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.
  Beki huyo aliyechezea kikosi cha Simba Wasiofungika kuanzia mwaka 1993 hadi 2010 akishinda mataji mawili ya AFCON na timu hiyo, enzi zake hizo aliwika klabu za Liverpool, Galatasaray, West Ham United na Metz.
  Jukumu la kwanza la Song, mjomba wa kiungo wa zamani wa Arsenal, Alex Song ni kuiongoza Chad katika ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Misri Jumatatu ya Novemba 9 nyumbani.
  Chad inatarajiwa kuikaribisha Tanzania Machi 25 katika mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kabla ya kurudiana mjini Dar es Salaam Machi 28.
  Alipokuja na Cameroon kama Meneja wa timu Februari mwaka 2013 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars, Song alifanya mazungumzo na Azam FC, kupitia kwa mmoja wa Wakurugenzi wake, Yussuf Bakhresa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RIGOBERT SONG KOCHA MPYA WA CHAD ITAKAYOMENYANA NA STARS MACHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top