• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 24, 2015

  ARSENAL YAPAA KILELENI LIGI KUU, KAZI IPO KESHO MAN UNITED NA MANCHESTER CITY

  MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA ENGLAND
  Leo Oktoba 24, 2015  
  Arsenal 2-1 Everton
  Norwich City 0-1 West Bromwich Albion
  Aston Villa 1-2 Swansea City
  Leicester City 1-0 Crystal Palace
  Stoke City 0-2 Watford
  West Ham United 2-1 Chelsea
  Kesho; Oktoba 25, 2015
  Sunderland Vs Newcastle United (Saa 10:00 jioni)
  Man United Vs Man City (Saa 12:05 jioni)
  Bournemouth Vs Tottenham (Saa 12:05 jioni)  
  Liverpool Vs Southampton (Saa 1:15 usiku)

  Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton. Kulia ni kipa Tim Howard wa Everton Uwanja wa Emirates leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  TIMU ya Arsenal imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton Uwanja wa Emirates usiku huu.
  Ushindi huo umeifanya Arsenal ifikishe pointi 22 baada ya kucheza mechi 10, ikiwazidi pointi moja Manchester City ambao kesho wanacheza mechi yao ya 10, dhidi ya mahasimu Manchester United.
  Mabao ya The Gunners katika mchezo wa leo yamefungwa na Olivier Giroud dakika ya 36 na Laurent Koscielny dakika ya 38, wakati bao pekee la Everton limefungwa na Ross Barkley dakika ya 44.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu ya England leo, Norwich City imelala 1-0 nyumbani mbele ya West Bromwich Albion, bao pekee la Salomon Rondon dakika ya 46 Uwanja wa Carrow Road.
  Swansea City imeshinda 2-1 ugenini mbele ya Aston Villa mabao ya Gylfi Sigurdsson dakika ya 68 na Andre Ayew dakika ya 87 Uwanja wa Villa Park, huku bao pekee la wenyeji likifungwa na Jordan Ayew dakika ya 62.
  Watoto wa Mwanasoka Bora wa zamani wa Afrika, Abedi Ayew 'Pele', Andre na Jordan Ayew wamekutana leo katika Ligi Kuu England na wote wamezifungia timu zao PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Leicester City imeshinda 1-0 dhidi ya Crystal Palace bao pekee la Jamie Vardy dakika ya 59 Uwanja wa King Power, wakati Watford imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Stoke City, mabao ya Troy Deeney dakika ya 43 na Almen Abdi dakika ya 69 Uwanja wa Britannia.
  West Ham United imewafunga mabingwa watetezi, Chelsea mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Mauro Zarate dakika ya 17 na Andy Carroll dakika ya 79, bao la The Blues likifungwa na Gary Cahill dakika ya 56 Uwanja wa Boleyn.
  Ligi Kuu ya England itaendelea kesho kwa mechi nne, macho ya wengi yakielekezwa kwa mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester, City na United Uwanja wa Old Trafford, wakati pia Sunderland itaikaribisha Newcastle United Uwanja wa Light, Bournemouth na Tottenham Hotspur Uwanja wa Vitality na Liverpool na Southampton Uwanja wa Anfield.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPAA KILELENI LIGI KUU, KAZI IPO KESHO MAN UNITED NA MANCHESTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top