• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 29, 2015

  AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI KUU, YANGA SC SASA WANAISOMA

  MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Oktoba 29, 2015
  Prisons 1-0 African Sports
  JKT Ruvu  2-4 Azam FC
  Oktoba 28, 2015
  Toto African 1-0 Mgambo Shooting
  Mwadui FC 2-2 Yanga SC
  Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar
  Mbeya City 1-1 Majimaji FC
  Ndanda FC 0-0 Stand United
  Simba Sc 1-0 Coastal Union
  Didier Kavumbangu (kushoto) akishangilia na Farid Mussa baada ya kufunga bao la kwanza leo

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-2 jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi nane, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga SC ambao jana walilazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui mjini Shinyanga.
  Kwa ushindi wa leo, sifa zimuendee mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu ambaye amefunga bao moja na kuseti mengine mawili, moja la John Bocco na lingine la Kipre Tchetche. 
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Israel Mujuni Nkongo, hadi mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
  Didier Kavumbangu akipiga shuti kufunga bao la pili pembeni ya beki wa JKT Ruvu, Michael Aidan
  John Bocco akimtoka Michael Aidan wa JKT Ruvu. Kushoto ni Kavumbangu  Mrundi Didier Kavumbangu alianza kufunga bao la kwanza dakika ya tano kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kiungo wa Ivory Coast, Kipre Michael Balou.
  Kavumbangu tena akamsetia Bocco krosi nzuri kufunga bao la pili dakika ya saba, kabla ya Najim Magulu kuifungia JKT Ruvu dakika ya 31.
  JKT walicharuka baada ya kupata bao na kupeleka mashambulizi ya nguvu langoni mwa Azam FC, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga.
  Kipindi cha pili, Azam FC ilikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 64, mfungaji Bocco kwa penalti baada ya beki wa JKT Ruvu, George Minja kumkwatua beki wa Azam FC, Shomary Kapombe.
  Kabla Azam FC hawajamaliza kushangilia bao lao la tatu, JKT Ruvu wakapata bao la pili dakika ya 69 kupitia kwa Emmanuel Pius aliyetumia makosa ya mabeki wa Azam FC kuchanganyana.
  Wakati JKT wapo kwenye jitihada za kusaka bao la kusawazisha, Azam FC walifanikiwa kupata bao la nne lililofungwa na Kipre Herman Tchetche aliyepokea pasi ya Kavumbangu.    
  Kikosi cha JKT Ruvu kilikuwa; Shaaban Dihile, Michael Aidan, Paul Mhidze, Renatus Morris, George Minja, Hamisi Shengo, Mussa Juma, Issa Ngao, Gaudence Mwaikimba/Samuel Kamuntu dk46, Najim Magulu/Abdulrahim Mussa dk73 na Saady Kipanga/Emmanuel Pius dk60.
  Azam FC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Said Mourad, Aggrey Morris, Serge Wawa, Kipre Bolou/Himid Mao dk46, Salum Abubakar `Sure Boy`, Jean Mugiraneza `Migi`, John Bocco `Adebayor`/Kipre Tchetche dk77, Didier Kavumbangu na Farid Mussa/Erasto Nyoni dk70.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI KUU, YANGA SC SASA WANAISOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top