• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 17, 2015

  RONALDO AWEKA REKODI MPYA YA MABAO REAL MADRID IKIUA 3-0

  MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo ameipiku rekodi ya gwiji wa Real Madrid, Raul baada ya kuifungia Real Madrid katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Levante mchezo wa la Liga leo Uwanja wa Santiago Bernabeu.
  Beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo alifunga bao la kwanza dakika ya 27, kabla ya Ronaldo kufunga la pili dakika tatu baadaye kwa shuti la mpira wa adhabu na Jesse kufunga la tatu dakika ya 81.
  Ronaldo sasa anafikisha mabao 324 katika mechi 310 tangu ajiunge na klabu hiyo, wakati Raul alifunga mabao 323 katika mechi 741.
  Ronaldo alikabidhiwa kiatu cha Dhahabu kabla ya mchezo huo kwa kuwa mfungaji bora wa Ulaya msimu uliopita PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AWEKA REKODI MPYA YA MABAO REAL MADRID IKIUA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top