• HABARI MPYA

    Friday, October 16, 2015

    ‘MIGI’ AREJEA USIKU KUIVAA YANGA SC KESHO TAIFA, KAPOMBE NAYE YUKO ‘FULL’

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza amewasili usiku wa kuamkia leo kutoka kwao Rwanda ambako alikwenda kuichezea timu yake ya taifa.
    Rwanda, Amavubi iliweka kambi ya siku 10 nchini Morocco kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Libya katikati ya Novemba na Jamanne ilifungwa 1-0 na kikosi cha Olimpiki cha Tunisia katika mchezo wake wa mwisho wa kujipima.
    Kikosi cha Amavubi Stars kimerejea jana Rwanda na Azam FC ikahakikisha mchezaji huyo hapotezi muda mrefu Kigali kabla ya kupanda ndege kuja Dar es Salaam kuuwahi mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga SC kesho.
    Mugiraneza (kulia) akiwa la Luckson Kakolaki, mmoja wa makocha Wasaidizi wa Azam FC

    Azam FC watakuwa na kibaruwa kizito mbele ya mabingwa watetezi, Yanga SC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema kwamba wako tayari kuelekea mchezo huo na lengo ni ushindi.
    “Sisi utaratibu wetu ni ule ule, kila mechi kwetu ni fainali, tunawaheshimu Yanga SC ni mabingwa, ni timu nzuri, lakini kesho tutajitahidi tuwafunge,”amesema. 
    Jaffar amesema kwamba beki Shomary Kapombe ambaye alirejea kutoka kuichezea timu ya taifa ya Tanzania akiwa majeruhi, amepona na yuko tayari kucheza kesho.
    Kapombe alimaliza dakika 90 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Malawi mjini Blantyre Jumapili kuwania kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia, lakini akatoka uwanjani anachechemea kwa maumivu ya mguu.
    Hali hiyo ilizua hofu kidogo labda beki huyo wa pembeni anaweza kuikosa mechi ya kesho- lakini sasa uongozi wa Azam FC unathibitiha yuko tayari kwa mtanange huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ‘MIGI’ AREJEA USIKU KUIVAA YANGA SC KESHO TAIFA, KAPOMBE NAYE YUKO ‘FULL’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top