• HABARI MPYA

  Sunday, October 25, 2015

  CANNAVARO: MBIO ZA UBINGWA NI YANGA SC NA AZAM FC TU

  MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Oktoba 28, 2015
  Toto African Vs Mgambo Shooting
  Mwadui FC Vs Yanga SC
  Mtibwa Sugar Vs Kagera Sugar
  Mbeya City Vs Majimaji FC 
  Ndanda FC Vs Stand United
  Simba SC Vs Coastal Union
  JKT Ruvu Vs Azam FC
  Oktoba 29, 2015
  Prisons Vs African Sports
  Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' kulia amesema mbio za ubingwa ni wao na Azam FC

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amesema kwamba ushindani wa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utaendelea kuwa baina yao na Azam FC msimu huu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jana, Cannavaro amesema kwamba baada ya raundi saba, Azam FC na Yanga SC zinakabana koo tena kileleni.
  “Unaweza kujionea mwenyewe, hatujapoteza mechi, na hawajapoteza. Mechi baina yetu tulitoka sare. Sasa sisi tunacheza tukiwafikiria wao, na wao wanacheza wakitufikiria sisi,”amesema.
  Cannavaro amesema kwamba wanatambua hawapaswi hata kutoa sare mechi yoyote, zaidi ya kushinda mfululizo iwapo wanataka kuipiku Azam FC katika mbio za ubingwa.
  Lakini Cannavaro anatambua kwamba Ligi Kuu ni ngumu kwa sababu timu nyingi ni nzuri, hivyo anawaambia wachezaji wenzake wanatakiwa kujituma kila mchezo.
  “Usione tunashinda ukadhani ligi nyepesi, hapana. Ligi ni ngumu sana, isipokuwa sisi kwa sababu tuna malengo tunajituma kila mechi. Wakati mwingine tunacheza na uchovu na maumivu, lakini huwezi kujua,”amesema.
  Nahodha huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars pia amesema mfano mchezo uliopita dhidi ya Toto African pamoja na kushinda 4-1, lakini waliingia wakiwa wamechoka kutokana na ugumu wa mchezo dhidi ya Azam FC ulioisha kwa sare ya 1-1.
  Yanga SC, ambao ndiyo mabingwa watetezi, wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao dhidi ya Azam FC wakiwa wanalingana kwa pointi, 16 kila mmoja.
  Yanga SC FC walitoka sare ya 1-1 wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa ‘live’ na Azam TV, inatarajiwa kuendelea Jumatano, Yanga SC wakisafiri hadi Shinyanga kwenda kumenyana na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, wakati Azam FC watamenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Toto African watakuwa wenyeji wa Mgambo Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa ndugu zao Kagera Sugar, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji FC Uwanja wa Sokoine, Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Stand United, Simba SC watakuwa wenyeji wa Coastal Union na Alhamisi Prisons watakuwa wenyeji wa African Sports.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CANNAVARO: MBIO ZA UBINGWA NI YANGA SC NA AZAM FC TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top