• HABARI MPYA

  Wednesday, October 28, 2015

  KIGODEKO AZIMA SHANGWE ZA YANGA KAMBARAGE, AWACHOMOLEA MWADUI DAKIKA ZA LALA SALAMA, SARE 2-2

  MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo Oktoba 28, 2015
  Toto African 1-0 Mgambo Shooting
  Mwadui FC 2-2 Yanga SC
  Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar
  Mbeya City 1-1 Majimaji Fc Sokoine
  Ndanda FC 0-0 Stand United
  Simba Sc 1-0 Coastal Union
  Oktoba 29, 2015
  Prisons        Vs African Sports
  JKT Ruvu    Vs Azam FC
  Donald Ngoma amefunga mabao yote ya Yanga SC ikitoa sare ya 2-2 na Mwadui

  Na Prince Akbar, SHINYANGA
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC, Bakari Kigodeko ameipokonya tonge mdomoni Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga baada ya kuifungia Mwadui FC bao la kusawazisha dakika la salama timu hizo zikitoka sare ya 2-2.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mzimbabwe Donald Ngoma alifunga mabao yote Yanga SC, moja kila kipindi.  
  Sare hiyo ya pili msimu huu, inawafanya mabingwa hao watetezi wafikishe pointi 20, baada ya mechi nane ingawa wanaendelea kuongoza Ligi Kuu, wakiizidi pointi moja Azam FC, ambayo kesho inacheza na JKT Uwanja wa Karume.   
  Yanga SC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nane mfungaji Donald Ngoma aliyemalizia pasi ya Mbrazil Andrey Coutinho.
  Mwadui walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 40 kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City, Paul Nonga ambaye mabeki wa Yanga walimuacha wakidhani ameotea.
  Kipindi cha pili, Ngoma alifunga dakika ya 75, kabla ya Kigodeko kuisawazishia Mwadui FC dakika ya 88.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Andrey Coutinho/Simon Msuva dk56, Thabani Kamusoko/Haruna Niyonzima dk80, Malimi Busungu/Deus Kaseke dk56, Amissi Tambwe na Donald Ngoma. 
  Mwadui FC; Shaaban kado, Shaaban Hassan, Malika Ndeule, David Luhende, Emmanuel Simwanda, Joram Mgeveke, Anthony Matogolo, Jamal Mnyate, Jabir Aziz/Athumani Iddi 'Chuji' dk70, Paul Nonga na Rashid Mandawa/Bakari Kigodeko dk67. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIGODEKO AZIMA SHANGWE ZA YANGA KAMBARAGE, AWACHOMOLEA MWADUI DAKIKA ZA LALA SALAMA, SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top