• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 22, 2015

  TAIFA STARS KUWEKA KAMBI DUBAI MAANDALIZI DHIDI YA ALGERIA KOMBE LA DUNIA

  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaweka kambi Afrika Kusini, Dubai au Oman kwa maandalizi ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria mwezi ujao.
  Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda amewaambia Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala mjini Dar es Salaam kwamba mipango inaendelea vizuri.
  "KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na hadi sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa,"amesema Teddy.
  Kikosi cha Taifa Stars kilichoitoa Malawi katika hatua ya kwanza ya mchujo wa Kombe la Dunia

  Katibu huyo, ametumia nafasi hiyo pia kutangaza namba za simu zitakazotumika kupokea michango ya Watanzania kwa ajili ya Taifa Stars.
  "Mtanzania yeyote anaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (Sh100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi," amesema.
  Teddy pia amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya mashabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
  Teddy Mapunda (kulia) akiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo

  "Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUWEKA KAMBI DUBAI MAANDALIZI DHIDI YA ALGERIA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top