• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 22, 2015

  AZAM FC YAIKALISHA NDANDA MTWARA NA KUIRUDIA YANGA JUU, KAZI IPO MWAKA HUU

  Na Mwandishi Wetu MTWARA
  BAO pekee la beki Shomary Salum Kapombe limeipa ushindi wa bao 1-0 Azam FC dhidi ya wenyeji, Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nangwanda, Sijaona, Mtwara.
  Kapombe alifunga bao hilo dakika ya 79 kwa kichwa akimalizia krosi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
  Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe poniti 19, sawa na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga SC wanaoendeleza kuongoza ligi hiyo kwa wastani wa mabao.
  Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Gadiel Michael, Aggrey Morris, Serge Wawa Pascal, Said Mourad, Frank Domayo, Himid Mao, Ame Ali ‘Zungu’/Khamis Mcha, Kipre Tchetche/Jean Mugiraneza na Ramadhani Singano ‘Messi’/John Bocco.
  Mechi nyingine za ligi hiyo leo, Mwadui FC wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
  Mabao ya Mwadui leo yamefungwa na Jerry Tegete dakika ya saba na 32 na Jamal Mnyate dakika ya 75, wakati bao pekee la Mgambo limefungwa na Abuu Daudi dakika ya 64.
  JKT Ruvu imetoka sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakati Mbeya City imeshinda 1-0 dhidi ya African Sports ya Tanga bao pekee la Geoffrey Mlawa dakika ya 15 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIKALISHA NDANDA MTWARA NA KUIRUDIA YANGA JUU, KAZI IPO MWAKA HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top