• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 28, 2015

  KIZZA DIEGO ‘MABAO’ ANARUDI MZIGONI LEO SIMBA IKIMENYANA NA COASTAL UNION TAIFA

  RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA WIKI HII
  Oktoba 28, 2015
  Toto African Vs Mgambo Shooting
  Mwadui FC Vs Yanga SC
  Mtibwa Sugar Vs Kagera Sugar
  Mbeya City Vs Majimaji FC
  Ndanda FC Vs Stand United
  Simba SC Vs Coastal Union
  Oktoba 29, 2015
  JKT Ruvu Vs Azam FC 
  Prisons Vs African Sports
  Hamisi Kiiza 'Diego' anatarajiwa kurejea uwanjani leo

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MCHEZAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwezi Septemba, Hamisi Friday Kizza ‘Diego’ yuko tayari kurudi uwanjani leo.
  Mganda huyo hajaonekana uwanjani tangu Simba SC ifungwe 2-0 na mahasimu, Yanga SC, Septemba 26, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini leo anaweza kurudi.
  Simba SC inamenyana na Coastal Union ya Tanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo Uwanja wa Taifa na Ofisa Habari wa Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema Kizza anaweza kurudi.
  “Kama mchezaji yuko fiti na amefanya mazoezi kikamilifu kuelekea mchezo huu, sasa ni jukumu la kocha mwenyewe kumuanzisha au la. Maana kocha wetu (Muingereza Dylan Kerr) naye ana maamuzi yake,”amesema.
  Mbali na Kizza, Manara amesema hata kiungo wao, Jonas Mkude naye yuko vizuri kabisa kuelekea mchezo wa leo na wanamuachia Kerr mwenyewe kama kawaida yake aamue wachezaji wa kutumia.
  Kwa ujumla Manara amesema Simba SC haina mchezaji majeruhi wala mgonjwa kuelekea mchezo wa leo na wanasubiri kuona kocha Kerr atawapangia timu ya aina gani leo.
  Kwa ujumla, Ligi Kuu inaendelea leo, mbali na Simba na Coastal- Mwadui FC inaikaribisha Yanga SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mgambo Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa ndugu zao Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro. 
  Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji FC Uwanja wa Sokoine, Ndanda FC wataikaribisha Stand United Uwanja wa Nangwanda, Mtwara wakati kesho JKT Ruvu watamenyana na Azam FC Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na Prisons wataikaribisha African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIZZA DIEGO ‘MABAO’ ANARUDI MZIGONI LEO SIMBA IKIMENYANA NA COASTAL UNION TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top