• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 19, 2015

  BIN ZUBEIRY ATEULIWA KAMATI YA TAIFA STARS KUELEKEA MECHI NA ALGERIA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MTENDAJI Mkuu wa BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE, Mahmoud Zubeiry ‘Bin Zubeiry’ ameteuliwa kwenye Kamati ya Uhamasishaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
  Akitaja Kamati hizo mchana wa leo katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa Stars, Farough Baghozah amesema kwamba lengo ni kuhakikisha maandalizi ya Taifa Stars yanakuwa mazuri katika kila eneo.
  Baghozah ameitaja Kamati ya Uhamasihaji chini ya Mwenyekiti Juma Abbas Pinto, ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA). 
  Wajumbe wa Kamati hiyo Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
  Mwenyekiti wa Kamati, Farough Baghozah (Katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo hoteli ya Serena. Kulia ni Katibu Teddy Mapunda na kushoto Makamu, Michael Wambura 

  Bin Zubeiry (kulia) akiwa na Katibu wa Kamati, Teddy Mapunda


  Kamati Kuu unaundwa na Mwenyekiti Farough Baghozah, Makamu wake Michael Wambura, Katibu Teddy Mapunda, Mweka Hazina, Wakili Imani Madega (Mweka Hazina), na Wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.
  Kama nyingine ndogo ni ya Maandalizi ya timu, chini ya Mwenyekiti wake, Madega na  Wajumbe Ahmed Mgoyi na Teddy Mapunda.
  Kamati ya Fedha Mwenyekiti wake,  Farough Baghozah na Wajumbe Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega, Juma Pinto, Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.
  Kamati ya Mikakati ya ushindi itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.
  Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii.  Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.
  Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.
  Aidha Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.  
  Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BIN ZUBEIRY ATEULIWA KAMATI YA TAIFA STARS KUELEKEA MECHI NA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top