• HABARI MPYA

  Monday, October 19, 2015

  AZAM FC WAIFUATA NDANDA MTWARA, YANGA WATAKUWA NA ‘TOTO LAO’ TAIFA JUMATANO, SIMBA WANABAKI MBEYA NA MAAFANDE

  MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
  Okotba 17, 2015
  Yanga SC 1-1 Azam FC
  Majimaji FC 1-0 African Sports
  Mbeya City 0-1 Simba SC
  Ndanda FC 0-0 Toto Africans
  Stand United 3-0 Prisons
  Coastal Union 0-1 Mtibwa Sugar
  Oktoba 18, 2015
  Mgambo Shooting 2-0 Kagera Sugar
  Mwadui FC 2-1 JKT Ruvu
  MECHI ZIJAZO..
  Oktoba 21, 2015
  Yanga SC Vs Toto Africans
  Stand United Vs Majimaji FC
  JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
  Prisons Vs Simba SC
  Coastal Union Vs Kagera Sugar
  Oktoba 22, 2015
  Ndanda FC Vs Azam FC
  Mwadui FC Vs Mgambo Shooting
  Mbeya City Vs African Sports
  Mziki wa Azam FC unahamia Nangwanda Sijaona Alhamisi dhidi ya Ndanda FC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Alhamisi dhidi ya wenyeji, Ndanda FC.
  Baada ya sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Yanga SC, Azam FC wamepania kufufua wimbi lao la ushindi keshokutwa mjini Mtwara.
  Azam FC ambao walilalamikia uchezeshaji mbovu wa refa Abadallah Kambuzi wa Shinyanga Jumamosi dhidi ya Yanga SC, wataendelea kumkosa kocha wao, Muingereza Stewart John Hall siku hiyo uwanjani kwa sababu bado anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa katka mchezo dhdi ya Coastal Union.
  Stewart atasafiri na timu na kuiandaa kama kawaida mazoezini, lakini siku ya mechi atakuwa jukwaani na mashabiki wengine kuangalia mchezo.
  Azam FC inafukuzana na Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu, kila timu ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, wakifuatiwa na Simba SC wenye pointi 15.
  Kwa ujumla, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea katikati ya wiki, Yanga SC wakiwakaribisha wanawe Toto Africans Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Stand United na Majimaji FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Prisons na Simba SC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Coastal Union na Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumatano.
  Ligi Kuu itaendelea tena Alhamisi, Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mwadui FC ikimenyana na Mgambo Shooting Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wakati Mbeya City watakuwa wenyeji wa African Sports ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAIFUATA NDANDA MTWARA, YANGA WATAKUWA NA ‘TOTO LAO’ TAIFA JUMATANO, SIMBA WANABAKI MBEYA NA MAAFANDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top