• HABARI MPYA

    Friday, October 16, 2015

    ANTHONY MARTIAL WA MAN UNITED AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI ENGLAND

    Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial baada ya kupokea tuzo yake Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    TAKWIMU ZA ANTHONY MARTIAL 
    MechiMabao
    Ligi Kuu43
    Ligi ya Mabingwa20
    Kombe la Ligi11
    TOTAL74
    MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Anthony Martial ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya England.
    Hiyo inafuatia Mfarabsa huyo kuisaidia Manchester United katika mechi zake za ligi hiyo mwezi uliopita baada ya kujiunga nayo msimu huu.
    Kinda huyo Mfaransa alijiunga na timu ya Old Trafford kutoka Monaco ya kwao kwa dau la Pauni Milioni 36 na akafunga mabao matatu mwezi uliopita.
    Martial alitokea benchi na kufunga katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Liverpool Uwanja wa Old Trafford katika ushindi wa 3-1 na kisha akafunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 ugenini dhidi ya Southampton. 
    Kinda huyo amewapiku mchezaji mwenzake wa United, Daley Blind, mshambuliaji wa Watford, Odion Ighalo, kipa wa Tottenham, Hugo Lloris, Dimitri Payet wa West Ham na mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy kutwaa tuzo hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANTHONY MARTIAL WA MAN UNITED AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top