• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 30, 2015

  ALGERIA YATAJA 33 WA AWALI KWA AJILI YA MECHI NA TAIFA STARS

  Sofiane Felghouli amejumuishwa kikosini
  TIMU ya soka ya taifa ya Algeria, imetangaza kikosi cha awali cha wachezaji 33 kwa ajili ya mchezo na Tanzania kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
  Kiungo mshambuliaji wa Leicester City aliye vizuri hivi sasa, Riyad Mahrez amejumuishwa katika kikosi hicho cha wachezaji 33 sambamba na Sofiane Felghouli ambaye ameripotiwa kuwaniwa na Manchester United na Chelsea za England pia.
  Wakali wengine kwenye kikosi hicho ni pamoja na Slimani Islam (Sporting Lisbon) na Bounedjah Baghdad wa Etoile du Sahel, ambayo iliitoa Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho mapema mwaka huu.
  Taifa Stars ambayo itamenyana na Algeria Novemba 14 mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana siku tatu baadaye mjini Algeirs na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia.
  Kikosi kamili cha awali cha Algeria ni; Doukha Azzedine ( JS Kabliye ), Ghoulam Faouzi ( Napoli –Italia), Riyad Mahrez (Leicester City –England ), Belfodil Ishak ( Beni Yas –UAE), Felghouli Sofiane ( Valencia – Hispania ), Brahimi Yacine (Porto – Ureno), Medjani Carl ( Trabzon Sport- Uturuki), Slimani Islam ( Sportin Lisbon- Ureno ), Bentaleb Nabil (Tottenham Hotspur – England ) na Soudani Hilal El Arabi (Dynamo Zaghreb,- Croatia ).
  Wengine ni Taider Sliti Saphir ( Bologna-Italia), Mandi Aissa (Stade Reims – Ufaransa), Kashi Ahmed (Charlton Athletic (Watford – England), Zeffane Medhi Embareck ( Stade Rennes – Ufaransa), Bounedjah Baghdad ( Etoile Du Sahel – Tunisia), Mesloub Walid (Lorrient – Ufaransa ), Boudebouda Brahimi ( USM Alger), Asselah Malik ( CR Belouizdade), Benayada Houcine (USM Alger ), Belkeroui Hichem ( Club African – Tunisia ), Hachoud Abderrahmen ( MC Alger ) na Khoualed Eddine of USM Alger.
  Wamo pia Mbolhi Rais ( Antalysapor – Turkey )Guedioura Adlane (Watford – England ), Mesbah Eddine ( Sampdoria –Italia), Abeid Mehdi (Panathinaikos –Ugiriki), Benrahma Said (GC Nice -Ufaransa), Jeaninin Mehdi (Paris Fc-Ufaransa), Ziti Khouthir (JS Kabliye ), El orfi Hoocine ( USM Alger), Ghezzal Rachid ( Olympique Lyon- Ufaransa).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALGERIA YATAJA 33 WA AWALI KWA AJILI YA MECHI NA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top