• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 24, 2015

  ANGOLA YAFUZU CHAN 2016 BAADA YA KUING'OA BAFANA BAFANA

  Angola imefuzu CHAN ya 2016 baada ya kuitoa Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2
  TIMU ya taifa ya Afrika Kusini imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Angola 2-1 Uwanja wa Novemba 11 mjini Luanda leo, lakini imetolewa katika mbio za kuwania tiketi ya fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika CHAN mwaka 2016 nchini Rwanda kwa jumla ya 3-2.
  Baada ya kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Rand wiki iliyopita, Bafana Bafana ilikwenda kupambana kiume ugenini kujaribu kupindua matokeo, lakini bahati haikuwa yao.
  Percy Tau alikuwa haba bahati baada ya mpira aliopiga kwa kichwa kuokolewa kwenye mstari, lakini Bafana Bafana wakapata bao karibu na mapumziko, baada ya mabeki wa Angola kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Lyle Lakay, kabla ya Gerson kuwasawazishia wenyeji.
  Lakay tena akaifungia Bafana Bafana bao la kipindi cha pili, lakini ni Angola inayofuzu CHAN ya mwakani Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ANGOLA YAFUZU CHAN 2016 BAADA YA KUING'OA BAFANA BAFANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top