• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 17, 2015

  SIMBA SC YANG’ARA LIGI KUU, YAICHAPA 1-0 MBEYA CITY SOKOINE, MAMBO YA JUUKO HAYO!

  MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA LEO
  Okotba 17, 2015
  Yanga SC 1-1 Azam FC
  Majimaji FC 1-0 African Sports
  Mbeya City 0-1 Simba SC
  Ndanda FC 0-0 Toto Africans
  Stand United 3-0 Prisons
  Coastal Union 0-1 Mtibwa Sugar
  KESHO; Oktoba 18, 2015
  Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar
  Mwadui FC Vs JKT Ruvu
  Juuko Murushid (kulia) leo ameing'arisha Simba SC Mbeya

  Na Princess Asia, MBEYA
  BAO pekee la beki Mganda, Juuko Murushid dakika ya tatu, limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Sokoine mjini hapa jioni ya leo.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi sita na kuendelea kuwa nafasi ya tatu, nyuma Yanga na Azam zenye pointi moja zaidi kila moja.
  Simba SC ilicheza vizuri leo na kama washambuliaji wake wangekuwa makini, wangeweza kuvuna mabao zaidi.
  Mshambuliaji Haruna Moshi aliichezea kwa mara ya kwanza leo Mbeya City tangu asajiliwe msimu huu na alidumu uwanjani kwa dakika 60 tu kabla ya kumpisha Hamad Kibopile.
  Kipa wa zamani wa timu ya vijana ya Chelsea ya England, Vincent Angban raia wa Ivory Coast leo aliidakia Simba SC kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu na kulinda vyema lango la Wekundu la Msimbazi.
  Hii inakuwa mara ya kwanza Simba SC kuifunga Mbeya City tangu ipande Ligi Kuu, msimu wa kwanza wakitoa sare mechi zote na msimu uliopita Wekundu wa Msimbazi wakifungwa mechi zote. 
  Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Yanga SC na Azam FC zimetoka sare ya 1-1, Majimaji FC imeifunga 1-0 African Sports, Ndanda FC imetoka sare ya 0-0 na Toto Africans, Stand United imeifunga 3-0 Prisons, Coastal Union imefungwa 1-0 na Mtibwa Sugar.
  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV, itaendelea kesho kwa michezo miwili, Mgambo Shooting na Kagera Sugar uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Mwadui FC na JKT Ruvu Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
  Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; Juma Kaseja, Hassan Mwasapile, John Kabanda, Haruna Shamte, Yohana Morris, Christan Sembuli/Abdallaha Seif dk46, Rafael Khalifa, Steven Banda, Haruna Moshi 'Boban'/Hamad Kibopile dk60, Themi Felix na Joseph Mahundi.
  Simba SC; Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude/Awadh Juma dk60, Justice Majabvi, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto/Joseph Kimwaga dk80, Mussa Hassan Mgosi na Abdi Banda/Peter Mwalyanzi dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YANG’ARA LIGI KUU, YAICHAPA 1-0 MBEYA CITY SOKOINE, MAMBO YA JUUKO HAYO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top