• HABARI MPYA

  Tuesday, October 20, 2015

  KIZZA 'DIEGO' AWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU SEPTEMBA

  Hamisi Kiiza
  MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
  Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa Sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
  Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi Tambwe).
  Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao matano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIZZA 'DIEGO' AWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU SEPTEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top