• HABARI MPYA

  Wednesday, October 21, 2015

  NGASSA: TAIFA STARS TUNAWEZA KUITOA ALGERIA MAANDALIZI YAKIWA MAZURI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesema inawezekana kuitoa Algeria kama kutakuwa na maandalizi mazuri.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwa simu kutoka Afrika Kusini, anakochezea klabu ya Free State Stars, Ngassa amesema kwamba Taifa Stars inaweza kuitoa Algeria ikiandaliwa vizuri.
  “Nimesoma wameunda Kamati na pia kuna mechi za Ligi Kuu (ya Vodacom Tanzania Bara) zimeahirishwa ili kutoa muda zaidi wa maandalizi kwa timu. Hizi ni hatua nzuri,”amesema Ngassa.
  “Nimesikia pia kuna mpango wa kambi ya nje ya nchi. Mimi kwa kweli naipongeza TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kwa hatua hizi, hata sisi wachezaji inatupa moyo,”amesema Ngassa.
  Mrisho Ngassa amesema Taifa Stars inaweza kuitoa Algeria ikiandaliwa vizuri 

  Hata hivyo, Ngassa mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar, Azam FC, Simba SC na Yanga amesema Kamati zilizoundwa zinapaswa kufanya shughuli zake vizuri na kwa umakini ili malengo yatimie.
  “Mimi ninaamini sisi kama wachezaji tutajituma na kujitolea kwa uwezo wetu wote kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,”amesema Ngassa.
  Tanzania itacheza mara mbili na Algeria ndani ya siku tatu nyumbani na ugenini kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
  Na TFF imeunda Kamati ya kusaidia maandalizi ya mchezo huo, chini ya Mwenyekiti Farough Baghozah, Makamu wake, Michael Wambura, Katibu Teddy Mapunda, Mweka Hazina Wakili Imani Madega na Wajumbe Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdallah na Musa Katabaro.
  Kamati hiyo nayo imeunda kamati ndogondogo ambazo ni Maandalizi ya timu, chini ya Mwenyekiti Wakili Madega na Wajumbe Ahmed Mgoyi, Teddy Mapunda, Kamati ya 
  Uhamasishaji wa mechi na Masoko chini ya Mwenyekiti Juma Pinto na Wajumbe Baraka Kizuguto, Mulamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon, Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
  Pia kuna Kamati ya Fedha, chini ya Baghozah mwenyewe na Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega, Juma Pinto, Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.
  Kuna Kamati ya Mikakati ya ushindi inayoundwa na Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Crescencius Magori.
  Kamati imeweka mikakati ya kukuanya fedha kwa ajili ya maandalizi ikiwemo kambi ya na kutangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” iliyoanza kutumika mara moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA: TAIFA STARS TUNAWEZA KUITOA ALGERIA MAANDALIZI YAKIWA MAZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top