• HABARI MPYA

  Wednesday, October 28, 2015

  KIZZA AREJESHA FURAHA SIMBA SC, MNYAMA ACHINJA WAGOSI TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la Mganda Hamisi Kizza ‘Diego’ limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kizza alifunga bao hilo baada ya kumchambua kipa wa Coastal Union, Fikirini Mapara kufuatia kupokea krosi maridadi ya Hassan Ramadhani Kessy kutoka upande wa kushoto.
  Baada ya bao hilo, Simba SC walijaribu kusaka mabao zaidi, lakini mabeki wa Coastal wakawa na kazi rahisi ya kumdhibiti mshambuliaji pekee wa timu hiyo, Kizza.
  Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Kizza baada ya kufunga bao pekee leo

  Kipindi cha pili, Coastal nao walikianza kwa kasi, lakini safu ya ulinzi ya Simba SC ilikuwa makini kuzuia hatari zote. 
  Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 18 baada ya mechi nane, na kupanda hadi nafasi ya tatu, nyuma ya Yanga na Azam.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Hassan Isihaka, Justice Majabvi, Said Ndemla, Jonas Mkude, Hamis Kizza/Mussa Mgosi dk74, Mwinyi Kazimoto na Peter Mwalyanzi/Ibrahim Hajib dk74.
  Coastal Union; Fikirini Mapara, Hamad Juma, Adeyoum Saleh, Abdallah Mfuko, Tumba Swedi, Yusuph Ssabo, Ibrahim Twaha ‘Messi’/Juma Mahadhi dk41, Mtenje Albano, Abasirim Chidiebere/Ayoub Semtawa dk46, Nassor Kapama na Ismail Mohammed.
  Kizza akikimbia kushangilia baada ya kufunga
  Hassan Kessy wa Simba SC akipiga krosi baada ya kumtoka beki wa Coastal Ismail Mohammed
  Kizza akiwatoka mabeki wa Coastal leo


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIZZA AREJESHA FURAHA SIMBA SC, MNYAMA ACHINJA WAGOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top