• HABARI MPYA

    Thursday, October 08, 2015

    STAND UNITED WAKOMA WENYEWE NA LIEWIG, WASEMA; "BABU MBISHI BALAA"

    Na Philipo Chimi, SHINYANGA
    MWENYEKITI wa klabu ya Stand United, 'Chama la Wana', Amani Vincent amemshutumu kocha Mkuu wa timu hiyo, Mfaransa Patrick Leiwig kwamba hataki ushauri wa viongozi na wasaidizi wake katika benchi la ufundi.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo mjini hapa, Amani amesema kwamba kocha huyo amekuwa akikaidi na kubeza ushauri unaotolewa na viongozi na hivi karibuni 'alitoleana maneno machafu' na Mwenyekiti huyo alipojaribu kumshauri jambo siku ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City mjini Shinyanga.
    Liewig ameingia kwenye mgogoro na Stand United kutokana na kutosikiliza ushauri wa uongozi

    "Kwa kweli huyu kocha sisi hatumuelewi, maana yeye ukitaka kumpa ushauri hataki, anataka yeye afanye anavyotaka, sasa hii inatupa shida kidogo, maana inasababisha tunashindwa kuelewena na makocha wenzake, lakini tutalifanyia kazi,”amesema Amani.
    Hivi karibuni Leiwig alipigwa faini ya Sh. Milioni 1 kufuatia kukiuka sheria za mchezo wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya African Sport, ikiwemo kugoma kuzungumza na Waandishi wa Habari.
    Tayari Liewig amemaliza adhabu yake baada ya kutokuwa katika benchi la Stand United kwenye mechi mbili, dhidi ya Simba SC Dar es Salaam timu ikifungwa 1-0 na Mbeya City mjini hapa timu ikishinda 1-0.
    Liewig aliyeajiriwa Stand United miezi miwili iliyopita, amewahi kufundisha Simba SC mwaka 2013 na huko alifukuzwa kwa tabia kama hizo, kutofuata ushauri wa uongozi.
    Uongozi wa Simba SC ulimshauri Liewig asimpange kipa Juma Kaseja katika mechi dhidi ya Yanga SC, lakini akampanga na baada ya timu kufungwa 2-0 katika mechi hiyo ya mwisho ya msimu, wote kocha huyo na kipa huyo hawakuongezewa mikataba. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED WAKOMA WENYEWE NA LIEWIG, WASEMA; "BABU MBISHI BALAA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top