• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 30, 2015

  KAVUMBANGU AWAWEKA MKAO WA KULA SIMBA SC, ASEMA AZAM FC…

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu amesema hataona sababu ya kubaki Azam FC iwapo kocha Muingereza, Stewart John Hall ataendelea kumuweka benchi.
  Baada ya kusoteshwa benchi kiasi cha kutosha msimu huu, Kavumbangu alipangwa jana Azam FC ikishinda 4-2 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na akafunga bao moja na kuseti mawili.
  Na baada ya mechi, Kavumbangu akaiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kama kocha Hall ataendelea kumuweka benchi basi hataona sababu ya kuendelea kubaki katika kikosi cha timu hiyo.
  Didier Kavumbangu akifurahia jana baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya JKT Ruvu

  Kavumbagu amesema anaweza kuondoka Azam FC katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo, Desemba endapo ataendelea kukaa benchi.
  Alisema anajiamini anaweza kucheza vizuri na kuisadia timu yake, hivyo kuendelea kusugua benchi itakuwa sawa na kumuonyesha mlango wa kutokea Chamazi.
  “Nashukuru kocha pamoja na benchi la ufundi kwa kunipa nafasi ya kucheza leo (jana), naamini kazi yangu, pia najiamini naweza kucheza mpira, hivyo kocha anatakiwa aniamini na kunipa nafasi ya kucheza,” amesema.
  “Sijazoea kukaa benchi, kwani ninaamini naweza kucheza na kuipatia ushindi timu yangu, hivyo ni jambo ambalo siwezi kukaa benchi kama itaendelea hivi, nitahama kwenda kucheza timu nyingine,” amesma.
  Wakati Kavumbangu akitoa msimamo huo, tayari kuna uvumi kwamba, wapinzaji wa Azam FC katika Ligi Kuu, Simba SC wanamtaka mchezaji huyo ‘kwa udi na uvumba’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAVUMBANGU AWAWEKA MKAO WA KULA SIMBA SC, ASEMA AZAM FC… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top