• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 17, 2015

  MANCHESTER ZOTE ZATOA VIPIGO ENGLAND, STERLING APIGA ‘HAT TRICK’ CITY YAUA 5-1

  Raheem Sterling akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Man City dhidi ya Bournemouth PICHA ZAIDI GONGA HAPA.

  JIJI la Manchester leo limegubikwa na furaha baada ya timu zote, City na United kung’ara katika Ligi Kuu ya England.
  Manchester City ndiyo imefanya ‘balaa kubwa’ baada ya kuichapa mabao 5-1 Bournemouth Uwanja wa Etihad, Raheem Sterling akifunga matatu peke yake.
  Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Sterling alifunga mabao yake dakika saba 29 na 48, wakati mabao mengine ya City yamefungwa na Wilfried Bony dakika ya 11 na 89, wakati la Bournemouth la kufutia machozi limefungwa na Glenn Murray dakika ya 22.
  Wayne Rooney akimaliza ukame wa mabao baada ya kumtungua Tim Howard katika ushindi wa 3-0 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mashetani Wekundu, Manchester United wameng’ara ugenini baada ya kuitandika Everton mabao 3-0 Uwanja wa Goodison Park, wafungaji  Morgan Schneiderlin dakika ya 18, Ander Herrera dakika ya 22 na Nahodha Wayne Rooney aliyeiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 62.
  Southampton imelazimishwa sare ya 2-2 Leicester City, mabao yake yakifungwa na Jose Fonte dakika ya 21 na Virgil van Dijk dakika ya 37, wakati ya wapinzani wao yamefungwa na Jamie Vardy dakika ya 66 na Jamie Vardy dakika ya 91 Uwanja wa St. Mary's.
  Nahodha wa Chelsea, John Terry (kulia) akienda hewani kugombea mpira na mshambuliaji wa Villa, Rudy Gestede PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mabingwa watetezi, Chelsea wameshinda 2-0 dhidi dhidi ya Aston Villa mabao ya Diego Da Silva Costa dakika ya 34 na Alan Hutton aliyejifunga dakika ya 54 Uwanja wa Stamford Bridge.
  West Ham United imeshinda ugenini 3-1 dhidi ya Crystal Palace, mabao yake yakifungwa na Carl Jenkinson dakika ya 22, Manuel Lanzini dakika ya 88 na Dimitri Payet dakika ya 94, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji limefungwa na Yohan Cabaye kwa penalti dakika ya 25 Uwanja wa Selhurst Park.

  Kocha mpya wa Liverpool, Jugern Klopp akitoa maelekezo kwa wachezaji wake Uwanja wa White Hart Lane PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kocha mpya wa Liverpool, Mjerumani Jurgen Klopp ameanza na sare tasa ugenini, baada ya kutoka 0-0 na Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane.
  Ligi Kuu ya England itaendelea kesho Newcastle United wakiikaribisha Norwich City Uwanja wa St. James' Park, wakati keshokutwa Swansea City watakuwa wenyeji wa Stoke City Uwanja wa  Liberty.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANCHESTER ZOTE ZATOA VIPIGO ENGLAND, STERLING APIGA ‘HAT TRICK’ CITY YAUA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top