• HABARI MPYA

  Friday, October 23, 2015

  NGASSA HATARINI KUWAKOSA ALGERIA, AUMIA NYAMA AFRIKA KUSINI, VIPIMO…

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa yuko hatarini kuukosa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria baada ya kuumia nyama. 
  Ngassa alicheza kwa dakika 63 tu kabla ya kumpisha Somaeb, klabu yake Free Free State ikishinda mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Polokwane City katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini Uwanja wa Old Peter Mokaba mjini Polokwane.
  Shukrani kwake, Andrea Fileccia aliyefunga mabao yote dakika za 82 na 89- na Ngassa alitoka uwanjani akiwa anachechemea juzi.
  Ngassa akihudumiwa na mchua misuli wa Free State

  “Nilitoka kwa sababu niliumia nyama, jana nimefanyiwa vipimo sasa nasubiri majibu kujua nini kitafuata. Lakini ninasikia maumivu makali sana,”amesema Ngassa akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS ONLINE leo kwa simu kutoka Afrika Kusini.
  Baada ya kuitoa Malawi kwa jumla ya mabao 2-1, wakishinda 2-0 Dar es Salaam mabao ya Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta na kufungwa 1-0 Blantyre, Taifa Stars watakutana na Algeria katikati ya mwezi ujao katika hatua ya mwisho ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la 2018 Urusi.
  Mrisho Ngassa sasa yuko hatarini kuikosa mechi dhidi ya Algeria
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA HATARINI KUWAKOSA ALGERIA, AUMIA NYAMA AFRIKA KUSINI, VIPIMO… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top