• HABARI MPYA

  Sunday, October 18, 2015

  YANGA SC NA AZAM FC KATIKA PICHA JANA TAIFA

  Mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu akipasua katikati ya wachezaji wa Azam FC, Serge Wawa (kuia) na Kipre Balou (kushoto) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
  Winga wa Azam FC, Farid Mussa (kulia) akiwafunga tela mabeki wa Yanga SC, Juma Abdul (katikati) na Nadir Haroub 'Cannavaro' (kushoto)
  Beki wa Azam FC, Serge Wawa (katikati) akipambana na washambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma (kulia) na Malimi Busungu (kushoto)
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu akimtoka beki wa Azam FC, David Mwantika
  Mshambuliaji wa Yanga SC, akiwatoka viungo wa Aam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Kipre Balou
  Kiungo wa Yanga SC, Thabani Kamusoko akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Azam FC, Aggrey Morris
  Kiungo wa Azam FC, Himid Mao akimgeuza kiungo wa Yanga SC, Thabani Kamusoko
  Beki wa Azam FC, David Mwantika akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga SC, Malimi Busungu
  Beki wa Yanga SC, Kevin Yondan akiondoka na mpira baada ya kumpokonya mshambuliaji wa Azam FC, Alan Wanga
  Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco akiwatoka wachezaji wa Yanga SC, Salum Telela na Donald Ngoma aliyeanguka chini
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC NA AZAM FC KATIKA PICHA JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top