• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 21, 2015

  MAGURI AENDELEA ‘KUWACHOMA ROHO’ SIMBA, APIGA MBILI STAND UTD YAUA 3-0 SHINYANGA

  MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
  Oktoba 21, 2015
  Yanga SC 4-1 Toto Africans
  Stand United 3-0 Majimaji FC
  JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
  Prisons 1-0 Simba SC
  Coastal Union 1-0 Kagera Sugar
  Kesho; Oktoba 22, 2015
  Ndanda FC Vs Azam FC
  Mwadui FC Vs Mgambo Shooting
  Mbeya City Vs African Sports
  JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
  Elias Maguri aliachwa Simba SC eti anakosa sana mabao, lakini sasa anafunga sana Stand United

  MSHAMBULIAJI Elias Maguri amezidi ‘kumsuta’ kocha Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr baada ya leo kufunga mabao mawili timu yake, Stand United ikishinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. 
  Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Maguri amefunga mabao mawili dakika za 47 na 60 timu yake, bao lingine likifungwa na Pastory Athanas dakika ya 66.
  Na Maguri sasa anafikisha mabao nane katika mechi nane za timu yake, akicheza saba tu, mchezo aliokosa ni dhidi ya Simba SC Dar es Salaam Stand ikilala 1-0. 
  Kocha alipendekeza Maguri aachwe katika usajili wa Simba SC msimu huu akidai eti anapoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Yanga SC imeifunga 4-1 Toto Africans, Prisons imeifunga 1-0 Simba SC na Coastal Union imeilaza 1-0 Kagera Sugar.
  Ligi Kuu itaendelea kesho, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Ndanda FC na Azam FC Mtwara, Mwadui FC na Mgambo Shooting Shinyanga na Mbeya City na African Sports Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAGURI AENDELEA ‘KUWACHOMA ROHO’ SIMBA, APIGA MBILI STAND UTD YAUA 3-0 SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top