• HABARI MPYA

  Saturday, October 31, 2015

  ARSENAL NA MAN CITY ZANG’ARA LIGI KUU ENGLAND, MAN UNITED YAAMBULIA SARE

  MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND LEO
  Novemba 31, 2015
  Crystal Palace 0-0 Manchester United
  Swansea City 0-3 Arsenal
  West Bromwich 2-3 Leicester City
  Newcastle United 0-0 Stoke City
  Watford 2-0 West Ham United
  Manchester City 2-1 Norwich City
  Chelsea 1-3 Liverpool
  Kesho; Novemba 1, 2015
  Everton Vs Sunderland (Saa 10:30 jioni)
  Southampton Vs Bournemouth (Saa 1:00 usiku)
  J’tatu Novemba 2, 2015
  Tottenham Hotspur Vs Aston Villa (Saa 5:00 usiku)
  Laurent Koscielny akishangilia baada ya kufunga bao la pili leo  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  TIMU ya Arsenal imeendelea ‘kula sahani moja’ na Manchester City kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Swansea City jioni ya leo Uwanja wa Liberty.
  Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Olivier Giroud dakika ya 49, Laurent Koscielny dakika ya 68 na Joel Campbell dakika ya 73 na sas Arsenal inafikisha pointi 25 sawa na Man City baada ya timu kucheza mechi 11, ingawa inabai nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.
  Michezo mingine ya ligi hiyo leo, Crystal Palace imelazimishwa sare ya 0-0 na Manchester United Uwanja wa Selhurst Park sawa na Newcastle United na Stoke City Uwanja wa St. James' Park.
  Leicester City imeshinda ugenini 3-2 dhidi ya West Bromwich Albion Uwanja wa The Hawthorns mabao yake yakifungwa na Riyad Mahrez dakika ya 57 na 64 na Jamie Vardy dakika ya 77, wakati ya wenyeji yamefungwa na Salomon Rondon dakika ya 30 na Rickie Lambert kwa penalti dakika ya 84.
  Beki wa kati wa Norwich, Ryan Bennett (katikati) akiteleza miguuni mwa mshambuliaji wa Manchester City, Bony PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mabao ya Odion Ighalo dakika ya 39 na 48 Uwanja wa Vicarage Road yameipa Watford ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United, wakati Manchester City imeshinda 2-1 dhidi ya Norwich City Uwanja wa Etihad, mabao yake yakifungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 67 na Yaya Toure kwa penalti dakika ya 89, huku la wageni likifungwa na Cameron Jerome dakika ya 83.
  Mchezo uliotangulia jioni ya leo, Chelsea imeendelea kuboronga baada ya kufungwa 3-1 nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge na Liverpool.

  Ramires Santos do Nascimento alianza kuifungia The Blues dakika ya nne, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 48 na kuifungia la pili dakika ya 74, huku la tatu likifungwa na Christian Benteke dakika ya 83.
  Winga wa zamani wa Man United, Zaha akijaribu kupasua katikati ya wachezaji wa timu hiyo, Marcos Rojo na Morgan Schneiderlin leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL NA MAN CITY ZANG’ARA LIGI KUU ENGLAND, MAN UNITED YAAMBULIA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top