• HABARI MPYA

  Sunday, October 25, 2015

  KOCHA MPYA LIVERPOOL ILE ILE, SARE TENA NA LEO 1-1

  TIMU ya Liverpool imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield.
  Hiyo inakuwa sare ya pili mfululizo kwa kocha mpya, Mjerumani Jurgen Klopp tangu arithi mikoba ya Brendan Rodgers aliyefukuzwa kwa mwenendo mbaya wa timu. Wiki iliyopita katika mechi yake ya kwanza Klopp Liverpool ilazimishwa pia sare ya 0-0 ugenini na Spurs.
  Katika mchezo wa leo, Liverpool ilitangulia kwa bao la Christian Benteke dakika ya 77, kabla ya  Sadio Mane kuwasawazishia wageni dakika ya 86.
  Mechi nyingine za leo, mahasimu wa Jiji la Manchester, United na City wametokq sare ya 0-0 Uwanja wa Old Trafford , wakati Spurs imeifumua 5-1 ugenini Bournemouth, Harry Kane akifunga mabao matatu kwa penalti dakika ya tisa, 56 na 63, mengine Mousa Dembele dakika ya 17 na Erik Lamela dakika ya 29.
  Bao pekee la wenyeji Uwanja wa Vitality limefungwa na Matt Ritchie dakika ya kwanza tu.
  Mshambuliaji Christian Benteke ametokea benchi na kuifungia Liverpool dhidi ya Southampton leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MPYA LIVERPOOL ILE ILE, SARE TENA NA LEO 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top