• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 29, 2015

  AZAM FC KUPANDA KILELENI LIGI KUU LEO?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iwapo itaifunga JKT Ruvu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
  Hiyo inafuatia mabingwa watetezi, Yanga SC kulazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jana.
  Na Azam FC wenye pointi 19, wataipiku Yanga SC inayoongoza kwa pointi 20 ligi hiyo hivi sasa.
  Hata hivyo, hilo halitarajiwi kuwa jambo jepesi, kwani JKT Ruvu haijashinda mechi hadi sasa msimu huu na inapambana na kujinusuru na balaa la kuwafuata ndugu zao, Ruvu Shooting Daraja la Kwanza.
  Kocha Stewart Hall (kushoto) na Wasaidizi wake katika benchi la Ufundi

  JKT Ruvu ililazimika kumuondoa kocha Freddy Felix Minziro na kumchukua mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ baada ya matokeo mabaya mfululizo.
  Na akiwa anaingia katika mchezo wake wa pili leo tangu aanze kazi, baada ya kutoa sare na Mtibwa Sugar wiki iliyopita, King Kibaden mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba anatarajiwa kumfurahisha mwajiri wake, Jeshi la Kujenga Taifa.
  Kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Joh Hall anataka kutumia vizuri mchezo wa leo kuwaacha Yanga SC kwa pointi baada ya kwenda nao ‘bega kwa bega’ tangu mwazo wa msimu.
  Lakini tayari kocha huyo wa zamani wa Sofapaka ya Kenya, amesema anamuhofia sana mshambuliaji wake wa zamani Azam FC, Gaudence Mwaikimba ambaye kwa sasa yuko JKT. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC KUPANDA KILELENI LIGI KUU LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top