• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 22, 2015

  NGASSA AENDELEA KUNG’ARA FREE STATE, YAITWANGA 2-0 TIMU YA PAPIC

  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa usiku huu ameiongoza klabu yake, Free State Stars kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Polokwane City Uwanja wa Old Peter Mokaba mjini Polokwane.
  Shukrani kwake, Andrea Fileccia aliyefunga mabao yote dakika za 82 na 89.
  Hata hivyo, mabao yote yalipatikana wakati Ngassa tayari yuko benchi, baada ya kutoka kumpisha Somaeb dakika ya 63.
  Free State imeshinda 2-0 dhidi ya timu ya Polokwane usiku huu

  Polokwane leo walicheza mechi ya kwanza baada ya kuachana na kocha wa zamani wa Yanga SC, Mserbia, Kosta Papic. 
  Kikosi cha Polokwane kilikuwa; Chigova, Phungwayo, Masenamela, Mbonani, Tema, Nene, Shiba/Ndou dk79, Maluleka, Alexander, Kanyenda/Mncwango dk63 na Tlolane.
  Stars: Diakite, Mashego, Sankara, Rakoti, Thlone, Ngassa/Somaeb dk63, Kerspuy, Masehe, Mohomi/Makhaula dk78, Venter na Fileccia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGASSA AENDELEA KUNG’ARA FREE STATE, YAITWANGA 2-0 TIMU YA PAPIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top