• HABARI MPYA

  Sunday, October 18, 2015

  RAIS KIKWETE: SIMBA NA YANGA ZINASAJILI KUUA VIPAJI KUKOMOA WACHEZAJI WANAOZISUMBUA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kwamba klabu kongwe nchini, Simba na Yanga husajili wachezaji wengine kwa kuwakomoa tu ili ziue vipaji vyao.
  Akizungumza katika hafla maalum ya kuagwa na Wanamichezo Jumatatu usiku ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Rais Kikwete anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu, alisema kwamba Simba na Yanga huwa zinasajili wachezaji zisizowahitaji, ili kuwakomoa.
  “Zikiona mchezaji anawasumbua sumbua, zinamsajili zinamuweka benchi msimu mzima, anaua kipaji chake halafu wanaachana naye,”alisema Rais Kikwete na kucheka.
  Rais Kikwete pia alipewa zawadi ya Ngao na Rais wa TFF, Jamal Malinzi

  Mapema wiki hii, Rais Kikwete alijichanganya na Wanamicheo katika sherehe iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
  Rais Kikwete alikabidhiwa tuzo maalum na TASWA kwa mchango wake katika michezo kwa kipindi cha miaka yake 10 ya utawala.
  Rais huyo naye akakabidhi tuzo kwa Wanamichezo 10 walioteuliwa na TASWA ambao walifanya vizuri katika kipindi cha miaka hiyo 10.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS KIKWETE: SIMBA NA YANGA ZINASAJILI KUUA VIPAJI KUKOMOA WACHEZAJI WANAOZISUMBUA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top