• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 19, 2015

  MZEE YUSSUF AFUNIKA ONYESHO LA KUFUNGA KAMPENI ZA FELA MBAGALA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WASANII wa muziki mbalimbali hapa nchini, juzi walitoa burudani ya aina yake katika mkutano maalum wa kufunga kwa kampeni ya Meneja na Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawawe na Wanaume Family TMK, Said Fella.
  Katika mkutano huo  Ya Moto bendi, Msanii Mkubwa kwa sasa hapa nchini Nasseb Abdul ‘Diamond Platinumz’ na Mfalme wa Taarabu Mzee Yusuph juzi walifunika katika hitimisho la kampeni za kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Kilungule Said Fella.
  Fella ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mkubwa na Wanawe yenye lengo kubwa la kuibua vipaji na kutoa ajira kwa vijana hapa nchini, juzi alihitimisha Kampeni zake za kuomba kura kwa wakazi wa Kata hiyo na kusindikizwa na wasanii mbalimbali hapa nchini.
  Mzee Yussuf akipagawisha wanachama wa CCM juzi kwenye kufunga kampeni za Said Fela

  Miongoni mwa wasanii waliotikisa katika Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Kilungule mwisho, ni Diamond anayetamba na kibao chake cha Nana baada ya kutangazwa kupanda jukwaani wakazi wa kata hiyo walizizima kwa shangwe kumshangilia nyota huyo.
  Mbali na Diamond pia kundi la Ya Moto bendi linalomilikiwa na Fella, nalo lilitikisa  huku wakazi wa kata hiyo wakiimba nao kwa pamoja wimbo unaotamba kwa sasa wa Cheza Kimadoido, huku pia Mzee Yusuph akiinua mwanzo mwisho wakazi waliojitokeza kusikiliza sera za Fella kupitia CCM.
  Wasanii wengine walioudhuria mkutano huo na kutoa burudani ni, Bushoke, Bonge la Nyau, Khalid Chokolaa, Bell Blacky, Mwasiti, Shetta, Mwana FA, Ditto pamoja na Ferouz aliyeliteka jukwaa pia kutokana na wananchi walivyomshangilia.
  Katibu Mwenezi wa CCm mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akimnadi Fela 

  Akizungumza na Wananchi Fella alisema, hajakurupuka kuwania nafasi hiyo, kwani ni mkazi wa KIlungule na shida zote katika Kata hiyo anazifahamu, huku akitolea mfano matatizo yanayowakabili wakazi wa Kata hiyo kuwa ni, Maji, Shule, Zahanati, Daraja na mambo mengine mengi ambayo anaimani wakimpa ridhaa atayatatua.
  Naye Mgombea Ubunge wa Mbagala Issa Mangungu aliwataka wananchi wa Kata hiyo, wasifanye makosa, kwani anamuamini Fella, kutokana na utendaji wake wa kazi kabla hata ya kujitosa kuwania nafasi hiyo, hivyo wakimpa ridhaa atahakikisha anasimamia maslahi ya wananchi kwa maendeleo ya wanakilungule.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MZEE YUSSUF AFUNIKA ONYESHO LA KUFUNGA KAMPENI ZA FELA MBAGALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top