• HABARI MPYA

    Saturday, October 03, 2015

    MOURINHO ‘AKARIBIA’ KUFUKUZWA, CHELSEA YACHAPWA 3-1 NYUMBANI NA SOUTHAMPTON

    MATOKEO MECHI ZILIZOMALIZIKA LIGI KUU ENGLAND:
    Chelsea 1-3 Southampton
    Manchester City 6-1 Newcastle United
    Crystal Palace 2-0 West Bromwich
    Norwich City 1-2 Leicester City
    Aston Villa 0-1 Stoke City
    AFC Bournemouth 1-1 Watford
    Sunderland 2-2 West Ham United
    Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akifoka kuwapa maelekezo wachezaji wake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    TIMU ya KOCHA Jose Mourinho sasa amekalia kitu kibovu na wakati wowote kinaweza kumdondosha darajani.
    Hiyo inafuatia Chelsea kufungwa mabao 3-1 nyumbani, Uwanja wa Stamford Bridge, London na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Mabingwa hao watetezi, The Blues ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Willian aliyefunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 10, kabla ya ‘Wakatifu’ kusawazisha kupitia kwa Steven Davis dakika ya 43 na Saido Mane kufunga la pili dakika ya 60 na Graziano Pelle la tatu dakika ya 72.
    Matokeo hayo yanaiangushia nafasi ya 16 Chelsea, inayomilikiwa na bilionea Mrusi, Roman Abramivic ambaye alishubhudia kipigo hiho leo Stamford Bidge.
    Katika mechi zilizotangulia Manchester City imerejea kileleni baada ya kuifunga Newcastle United mabao 6-1 jioni ya leo Uwanja wa Etihad.
    Mshambuliaji wa Argentina, Sergio ‘Kun’ Aguero amefunga mabao matano katika ushindi huo dakika za 42, 49, 50, 60 na 63, huku bao lingine la Man City likifungwa Kevin De Bruyne dakika ya 53.
    Bao pekee la Newcastle, limefungwa na Mserbia Aleksandar Mitrovic dakika ya 18 na sasa City inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi nane, mbili zaidi ya Manchester United waliocheza mechi saba.
    Mechi nyingine za Ligi Kuu zilizomalizika Crystal Palace imeshinda 2-0 dhidi ya West Bromwich, Leicester City imefungwa 2-1 nyumbani na Norwich City, Aston Villa imefungwa 1-0 nyumbani na Stoke City, AFC Bournemouth imelazimishwa sare ya 1-1 na Watford, Sunderland imetoka 2-2 na West Ham United.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOURINHO ‘AKARIBIA’ KUFUKUZWA, CHELSEA YACHAPWA 3-1 NYUMBANI NA SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top