• HABARI MPYA

    Thursday, October 08, 2015

    HARAMBEE STARS YAWAPIGA 5-2 MAURITIUS KWAO, BURUNDI NAYO YASHINDA UGENINI

    MATOKEO MECHI ZA MCHUJO KUFUZU KOMBE LA DUNIA
    Mauritius 2-5 Kenya
    Shelisheli 0-1 Burundi
    Tanzania 2-0 Malawi
    Comoro 0-0 Lesotho
    MECHI ZIJAZO
    Oktoba 8, 2015
    Sudan Kusini v Mauritania
    Sao Tome v Ethiopia
    Liberia v Guinea-Bissau
    Oktoba 9, 2015
    Somalia v Niger
    Djibouti v Swaziland
    Gambia v Namibia
    Oktoba 10, 2015
    Afrika ya Kati v Madagascar
    Chad v Sierra Leone
    Eritrea v Botswana

    KENYA, Harambee Stars jana imeanza vizuri harakati za kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi, baada ya kuwafunga mabao 5-2 wenyeji Mauritius katika mchezo wa kwanza wa mchujo Uwanja wa Stade Anjalay mjini Belle Vue Maural.
    Mabao ya Stars jana yamefungwa na Johanna Omollo mawili, Ayub Timbe, Harun Shakava na Michael Olunga, wakati mabao ya Mauritius yalifungwa na Jean Steve Jonathanna Kevin Bru na sasa Kenya watakuwa na mchezo laini wa marudiano nyumbani Jumapili.
    Mechi nyingine za kwanza za mchujo jana, Burundi imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Shelisheli Uwanja wa People, Comoro imelazimishwa sare ya 0-0 na Lesotho.
    Mechi za kwanza za mchujo zinaendelea leo, Sudan Kusini wakiwa wenyeji wa Mauritania huko  Juba, Sao Tome e Principe na Ethiopia, Liberia na Guinea-Bissau, Somalia na Niger, Djibouti na Swaziland, Gambia na Namibia wakati Jumamosi Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) itamenyana na Madagascar, Chad v Sierra Leone na Eritrea na Botswana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HARAMBEE STARS YAWAPIGA 5-2 MAURITIUS KWAO, BURUNDI NAYO YASHINDA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top