Na Mahmoud Zubeiry, DAR E3S SALAAM
MSIMU wa 2010/2011 Simba SC ilimsajili mshambuliaji chipukizi, Mbwan Ally Samatta kutoka African Lyon ya Dar es Salaam iliyokuwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pia.
Lakini mchezaji huyo baada ya kufanya mazoezi na timu hiyo kwa wiki kadhaa, akarudi zake nyumbani na kujitoa kabisa kikosini.
Alipoulizwa sababu, akasema hajatekelezewa mahitaji yake aliyoahidiwa wakati anasajiliwa- kupewa gari aina Toyota Mark II GX100 na fedha Sh. Milioni 5 kama sikosei.
Wengi kati ya waliokuwa watu wa karibu wa Mbwana waliokuwa wanatambua kipaji chake, walimsihi akajiunge na timu ili kukuza kipaji chake.
Lakini mshambuliaji huyo alishikilia msimamo wake wa kutojiunga na Simba hadi apewe chake.
Baada ya Simba SC kumuona Mbwana akicheza vizuri timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes wakajishusha wakaenda kumpa walivyomuahidi naye mwishoni mwa mwaka 2010 akajiunga na timu.
Mwanzoni mwa mwaka 2011, Simba SC ikamuuza Mbwana Samatta kwa Sh. Milioni 100 TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Na Mkataba wa mauziano ambayo Simba SC ilisaini na Mazembe chini ya aliyekuwa Rais wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage ni kwamba, Samatta akiuzwa nao watapata mgawo.
Na Samatta atauzwa, tena kwa dau zuri muda si mrefu, Simba itanufaika tena.
Katika dirisha dogo la usajili, Desemba mwaka jana, Simba SC ilisajili beki hodari wa kulia, chipukizi Hassan Ramadhan Kessy kutoka Mtibwa Sugar.
Baada ya kijana huyo kucheza Simba SC tangu Desemba tena akiwafurahisha mashabiki wa timu hiyo kwa soka yake nzuri ya kuzuia na kushambulia, mwezi uliopita akajitoa kikosini na kurejea kwao, Morogoro.
Alipoulizwa sababu, naye kama Samatta akasema hajatekelezewa mahitaji yake, anadai hajamaliziwa fedha za usajili na hajapewa nyumba ya kuishi kama alivyoahidiwa.
Ameamua kurudi nyumbani na yuko tayari kurejea kazini wakati wowote akitekelezewa mahitaji yake.
Msimamo wa Kessy ni aina ya misimamo ambayo wanayo watu wenye kujiamini tu. Ni msimamo ambao alikuwa nao hata Mbwana Samatta. Na kuna imani, watu wenye kujiamini Mungu huwafungulia njia. Bila shaka, naye Kessy anamuamini Mungu wake. Kama ipo ipo tu.
Inaonyesha Kessy si aina ya wachezaji ambao wako tayari kukaa benchi, au kucheza bila malipo, kisa yupo timu kubwa, Simba au Yanga.
Mkwara wa Simba SC eti itamfungia mchezaji hata kama madai yake ni ya msingi, hauna maana kwa sababu kati ya pande hizo mbili kuna Mkataba.
Mwajiri pia asipotekeleza Mkataba anaweza kuwa chanzo cha Mkataba kuvunjika. Pande zote mbili zinazotia saini Mkataba zinapaswa kuuheshimu.
Je, nani ameupuuza Mkataba waliosaini baina yao kati ya Simba na Kessy?
Mchezaji amecheza tangu Desemba hadi Machi mwishoni anakuja kugoma. Maana yake amevumilia. Mchezaji hajapewa nyumba ya kuishi tangu Desemba, anaishije?
Hii inaonyesha uongozi wa Simba SC hauko makini katika kutekeleza stahiki za wachezaji wake, jambo ambalo si zuri. Ilitokea kwa Mbwana Samatta, na sasa inajirudia kwa Kessy, klabu ile ile, japokuwa sasa hivi Rais si Rage, ni Evans Aveva. Simba, wana matatizo. Wabadilike.

| Hassan Kessy akiichezea Simba SC dhidi ya JKT Ruvu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu |

![]() |
| Mbwana Samatta aligoma kujiunga na Simba SC hadi apewe stahiki zake |
Inaonyesha Kessy si aina ya wachezaji ambao wako tayari kukaa benchi, au kucheza bila malipo, kisa yupo timu kubwa, Simba au Yanga.
Mkwara wa Simba SC eti itamfungia mchezaji hata kama madai yake ni ya msingi, hauna maana kwa sababu kati ya pande hizo mbili kuna Mkataba.
Mwajiri pia asipotekeleza Mkataba anaweza kuwa chanzo cha Mkataba kuvunjika. Pande zote mbili zinazotia saini Mkataba zinapaswa kuuheshimu.
Je, nani ameupuuza Mkataba waliosaini baina yao kati ya Simba na Kessy?
Mchezaji amecheza tangu Desemba hadi Machi mwishoni anakuja kugoma. Maana yake amevumilia. Mchezaji hajapewa nyumba ya kuishi tangu Desemba, anaishije?
Hii inaonyesha uongozi wa Simba SC hauko makini katika kutekeleza stahiki za wachezaji wake, jambo ambalo si zuri. Ilitokea kwa Mbwana Samatta, na sasa inajirudia kwa Kessy, klabu ile ile, japokuwa sasa hivi Rais si Rage, ni Evans Aveva. Simba, wana matatizo. Wabadilike.

.png)
0 comments:
Post a Comment