• HABARI MPYA

    Monday, August 11, 2014

    ARTETA NAHODHA MPYA ARSENAL, MSAIDIZI WAKE MERTESACKER

    KOCHA Arsene Wenger amemthibitisha Mikel Arteta kuwa Nahodha mpya wa Arsenal kufuatia kumuuza Thomas Vermaelen kwa Barcelona FC.
    Kocha huyo wa The Gunners, ambaye aliishuhiudia timu yake ikiwafumua mabao 3-0 mabingwa wa England, Manchester City katika mchezo wa Ngao ya Jamii jana, alilazimika kuwa na Nahodha mpya baada ya aliyekuwa Nahodha wake, Vermaelen kutimkia Barcelona.
    Mustakabli wa Arteta katika klabu bado hauko wazi sana, lakini inaonekana kwa kukabidhiwa uongozi wa wachezaji wenzake, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atabaki Arsenal msimu huu. Per Mertesacker ameteuliwa kuwa Nahodha Msaidizi.
    Cheo: Mikel Arteta amateueliwa kuwa Nahodha mpya wa Arsenal
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARTETA NAHODHA MPYA ARSENAL, MSAIDIZI WAKE MERTESACKER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top