• HABARI MPYA

    Tuesday, July 01, 2014

    SUAREZ AOMBA RADHI KWA KUMNG'ATA CHIELLINI, YADAIWA BARCELONA IMEMLAZIMISHA ILI AHAMIE CAMP NOU

    MSHAMBULIAJI Luis Suarez amepoza shutuma dhidi yake baada ya Jumatatu usiku kuomba radihi kwa kumng'ata Giorgio Chiellini na ameahidi kutorudia kufanya kosa kama hilo - huku Barcelona ikipiga hatua zaidi katika kuwania saini yake.
    Siku nne baadea ya kufungiwa miezi minne na ameambia FIFA kwamba tukio hilo lilitokea katika mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italua mjini Natal lilitokana na kushindwa kujizuia.
    Mshambuliaji huyo wa Liverpool ameibuka kikamilifu na kujutia kosa lake. Lakini kuomba kwake radihi kunakuja katika wiki ambayo habari zimevuma mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatakiwa kwa dau la Pauni Milioni 80 Nou Camp.
    Gary Lineker, mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, amesema klabu hiyo ya Katalunya imemuambia Suarez bombe msamaha kama wanataka waendelee na jitihada za kumnunua.
    Msamaha: Hatimaye Luis Suarez amoeba radihi kwa kumng'ata beki wa Italian wiki iliyopita
    Thumbs up: Luis Suarez gestures to fans from the balcony of his home, near Montevideo
    Dole tupu: Luis Suarez akiwapungia mashabiki katika juu ya nyumbani kwake karibu na Montevideo

    Katika taarifa yake aliyoitoa kwenye ukurasa wake wa Twitter, Suarez amesema: "Baada ya siku kadhaa za kuwa nyumbani na familia yangu, nimepata fursa ya kutuliza jazba na kufikiria haswa kilichotokea katika mechi ya Italia na Uruguay Juni 24, 2014.
    "Kutokana na kilichotokea na yote yaliyofuatia baadaye, kiasi cha kuathiri hata kiwango cha timu yangu ya taifa, ukweli ni kwamba mchezaji mwenzangu Giorgio Chiellini ameumizwa na kilichotokea kwa kumng'ata,".
    "Kwa hili: Najuta kwa kiasi kikubwa kufanya hivyo. Naomba radhi kwa Giorgio Chiellini na familia ya soka kwa ujumla. nauambia umma kwamba halitatokea tukio kama hili tena,".
    Beki wa Juventus, Chiellini ameretweet msamaha wa Suarez katika mtandao wake, baada ya awali kusema adhabu ya kumfungia miezi minne Suarez ni kubwa. 
    Chiellini amejibu kwenye akaunti yake ya Tweeter moja kwa moja akisema: "Yote yamesahaulika. Natumai FIFA itakupunguzia adhabu,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AOMBA RADHI KWA KUMNG'ATA CHIELLINI, YADAIWA BARCELONA IMEMLAZIMISHA ILI AHAMIE CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top