• HABARI MPYA

    Monday, December 09, 2013

    SZCZESNY AANIKA PENZI LAKE SHATA SHATA NA 'KIMODO' CHA POLAND KINACHOTISHA KWENYE MUZIKI NA FILAMU PIA

    KIPA wa Arsenal, Wojciech Szczesny amekuwa kivutio katika kikosi cha The Gunners msimu huu na uhusiano wake mpya na mlimbwende wa Poland, Marina Luczenko unaweza kuwa chachu. 
    Kufuatia sare ya 1-1 ya Arsenal na Everton Jumapili, mzuia michomo huyo wa Poland ameposti kwenye ukurasa wake wa Facebook picha akiwa na mpenziwe, Luczenko.
    Szczesny pia ameposti pia ujumbe mfupi, lakini mtamu wa mapenzi pamoja na picha. 
    Penzi changa: Wojciech Szczesny (kushoto) na Marina Luczenko wametoa picha hii kutangaza wapo kwenye mahusiano ya kimepanzi
    Musician: Luczenko has released several singles and unveiled her debut album in November
    Mwanamuziki: Luczenko ametoa nyimbo kadhaa kabla ya kutambulisha albamu yake ya kwanza, Novemba

    Ameandika: "Furaha...na Marina Luczenko".
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anatumaini kudumu na mpenzi wake, Luczenko, ambaye anafahamika sana nchini kwao, Poland kama msanii wa muziki, mwanamitindo na mwigizaji.
    Wachezaji kadhaa wa timu ya taifa ya Poland wamefurahia mahusiano ya wawili hao wakiwemo Robert Lewandowski na Kuba Błaszczykowski ambao wali-like posti hiyo kwenye Facebook.  
    Celebrity: Luczenko (left) is a well known musician, model and actress in Poland
    Maarufu: Luczenko (kushoto) anafahamika vyema kama mwanamuziki, mwanamitindo na mwigizaji Poland
    No 1: Polish star Luczenko announced she is dating Szczesny via her official Facebook page
    Namba 1: Nyota wa Poland, Luczenko ametangaza anatembea na Szczesny kupitia ukurasa wake wa Facebook
    Stopper: Wojciech Szczesny has helped his Arsenal side to the top of the Barclays Premier League
    Mzuia michomo: Wojciech Szczesny ameisaidia Arsenal kujinafasi kileleni mwa Ligi Kuu England msimhu huu hadi sasa
    Safe hands: Wojciech Szczesny clears an Everton attack during the 1-1 draw at the Emirates Stadium
    Mikono salama: Wojciech Szczesny akiokoa hatari langoni wakati wa mechi dhidi ya Everton iliyoisha kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Emirates
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SZCZESNY AANIKA PENZI LAKE SHATA SHATA NA 'KIMODO' CHA POLAND KINACHOTISHA KWENYE MUZIKI NA FILAMU PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top