• HABARI MPYA

    Sunday, December 01, 2013

    AZAM WA TATU KOMBE LA UHAI

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    AZAM FC imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Bara, maarufu kama Kombe la Uhai, baada ya kuifunga kwa penalti 3-1 Mtibwa Sugar kufuatia sare ya 3-3 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
    Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2 na zilipoongezwa dakika 30 kila timu ikapata bao moja zaidi.

    Mabao ya Azam yalifungwa na Eric Haule dakika ya 32, Adam Omary dakika ya 38 na Ahmed Abbas dakika ya 109, wakati mabao ya Mtibwa yalifungwa na Ally Makarani dakika ya 16, Hassan Mbande dakika ya 81 na Issa Kiganga kwa penalty dakika ya 105.
    Penalti za Azam zilifungwa na Mgaya Abdul, Shiraz Abdallah na Ahmed Abbas, wakati ya Mtibwa ilifungwa na Jumanne Mlindwa.
    Fainali ya michuano hiyo inachezwa jioni hii ikizukutanisha Yanga na Coastal Union Uwanja huo huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM WA TATU KOMBE LA UHAI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top