• HABARI MPYA

    Friday, March 02, 2012

    SPURS WAPANIA KUIFUNGA KWA MARA YA KWANZA MAN UNITED ZAIDI YA MIAKA 10


    KLABU ya Tottenham Hotspur imedhamiria kuifunga Manchester United kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 10 wakati timu hizo zitakapokutana kwenye Uwanja wa White Hart Lane Jumapili, ikifahamika kwamba wanatakiwa kujikaza baada ya kudundwa na Arsenal katika mechi iliyopita.
    Katika mechi hiyo dhidi ya United inayoshika nafasi ya pili, ikiwazidi Spurs wanaoshika nafasi ya tatu pointi nane, Tottenham watawatumia kiungo Gareth Bale, mshambuliaji Rafael van der Vaart na beki wa pembeni Kyle Walker ambao walikuwa majeruhi na sasa wamepona.
    Man United wanazidiwa pointi mbili na vinara Manchester City.
    Kocha Harry Redknapp lazima aizindue timu yake kutoka kwenye kipigo cha mabao 5-2 walichopewa na wapinzani wao katika jiji la London, Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates Jumapili iliyopita, lakini kwa bahati mbaya watamkosa Nahodha mpya wa England, Scott Parker ambaye anatumikia adhabu.
    Alipoulizwa kama Tottenham wapo kwenye nafasi nzuri ya kuwafunga United tangu walipoifunga mara ya mwisho mwaka 2001, Redknapp alisema: "Bado ni ngumu. Manchester United bado ni timu kubwa,”alisema.
    Spurs inawazidi wapinzani wao katika jiji la London, Arsenal na Chelsea kwa pointi saba katika vita ya kuwania nafasi ya tatu, ambayo moja kwa moja inatopa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa na Redknapp alisema kwamba kipaumbele kilikuwa ni kutwaa taji la Ligi kwa mara ya kwanza tangu 1961, ingawa sasa matumaini yamepungua kutokana na matokeo yao ya karibuni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPURS WAPANIA KUIFUNGA KWA MARA YA KWANZA MAN UNITED ZAIDI YA MIAKA 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top