• HABARI MPYA

    Friday, March 02, 2012

    WACHOVU KIYOVU WATUA DAR, SIMBA WAKUSANYA WA KIMATAIFA WOTE BAMBA BEACH


    WAPINZANI wa Simba SC katika Kombe la Shirikisho, Kiyovu Sport ya Rwanda wamewasili leo tayari kwa mechi ya marudiano ya Raundi ya Kwanza dhidi ya Wekundu wa Msimbazi.
    Kiyovu wanawasili wakati wenyeji wao Simba, wamekusanya wachezaji wao wote waliokuwa timu za taifa za Uganda na Tanzania kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani na kuwaunganisha kambini na wenzao Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam.
    Timu hizo zilizotoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Kigali, Rwanda, zinatarajiwa kurudiana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Wachezaji wa Simba ambao waliokuwa timu za taifa ni Juma Kaseja,  Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Jonas Gerald, Nassor Masoud ‘Chollo’, Shomari Kapombe,  Mwinyi Kazimoto na Uhuru Suleiman waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichotoa sare ya 1-1 na Msumbiji na Emanuel Okwi aliyekuwa kwenye kikosi cha Uganda kilichofungwa 3-1 na Kongo Brazzaville.
    Mechi hiyo itaanza saa 9.30 alasiri na itachezeshwa na refa Yabarow Hagi Wiish atakayesaidiwa na Aweis Ahmed Nur na Abdirahman Omar Abdi, wote kutoka Somalia, wakati refa wa akiba atakuwa Waziri Sheha wa Tanzania na Kamisaa Jean Marie V. Hicuburundi kutoka Burundi.
    Watazamaji watatakiwa kulipa Shilingi 30,000 kwa kwa viti vya VIP A, 20,000 kwa VIP B, 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya Chungwa ni Sh.8,000 na rangi ya bluu na kijani Shilingi 5,000.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHOVU KIYOVU WATUA DAR, SIMBA WAKUSANYA WA KIMATAIFA WOTE BAMBA BEACH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top