• HABARI MPYA

    Saturday, March 03, 2012

    KIIZA FIFTY FIFTY KUCHEZA LEO

    HAMIS Kiiza alizua hofu kwa Yanga juzi jioni baada ya kuumia na kutolewa nje mazoezini, lakini benchi la ufundi limesema uwezekano wa nyota huyo kucheza leo upo.
    Raia huyo wa Uganda aliyefunga bao pekee katika sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam dhidi ya Zamalek ameonekana mchangamfu sana kambini na asiye na mzongo wa mawazo kama baadhi ya wachezaji wengine wa Yanga.
    Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro alisema,"alikuwa na tatizo la nyonga tangu Dar es Salaam sasa kutokana na baridi kuwa kali akajitonesha, lakini amerudi kwenye hali ya kawaida na tunatarajia kumtumia."
    Ingawa Minziro alisema lolote linaweza kutokea kwenye mazoezi ya leo jioni kwenye Uwanja wa Chuo Cha Jeshi la Misri kutokana na hali ya hewa na mazingira wakabadili kikosi cha kwanza.
    Huenda kocha akamuanzisha Tegete na kumuweka nje Asamoah kwa madai kuwa akiingia kipindi cha pili huwa anakuwa fiti zaidi na mwenye madhara makubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA FIFTY FIFTY KUCHEZA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top