• HABARI MPYA

    Saturday, March 03, 2012

    ANGETILE SASA 'ALHAMDULILLAH'

    HALI ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji Jumatano iliyopita kwenye Hospitali ya Apollo nchini India.
    Akizungumza jijini jana Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema Osiah anaendelea vizuri na atakuwa kwenye chumba maalumu kwa muda wa siku sita na baadaye kuhamishiwa kwenye wodi kwa muda wa siku 16.
    Wambura alifafanua kuwa kwa ujumla matibabu yake yatachukua muda wa mwezi mmoja.
    Katibu Mkuu huyo aliondoka nchini Februari 23 kuelekea nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa baada ya kubainika kuwa alikuwa na uvimbe. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANGETILE SASA 'ALHAMDULILLAH' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top